HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 4, 2017

MC ALGER KUTUA ALHAMIS USIKU, YANGA YAJIZATITI KUBAKISHA USHINDI NYUMBANI



Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya MC Alger ya Algeria wa hatua ya mtoano wa kombe la Shirikisho.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Wapinzani wa Yanga katika mtuano ya kombe la Shirikisho badani Afrika kutoka nchini Algeria, MC Alger wanatarajiwa kuingia nchini siku ya Alhamis wakiwa na msafara wa watu 40 .

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio huo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kuwa wametumiwa taarifa kuwa timu hiyo itawasili majira ya saa 3 usiku kutoka nchini Algeria.

Mkwasa amesema kuwa, kuelekea mchezo huo utakaochezwa Jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa utakuwa wa ushindani mkubwa sana kwani wanazifahamu vizuri timu za kiarabu.

Amesema kuelekea mchezo huo kwa sasa benchi la ufundi linaendelea kuwapa wachezaji mbinu mbalimbali na tayari wameshaanza mazoezi na wameingia kambini kwa ajili ya kupata umakini zaidi.



" timu yetu kwa sasa inaongoza ligi na tupo katika njia nzuri za kuutetea ubingwa wetu. Hawa wanaoleta maneno ya uzushi hawana nia njema na klabu , wanataka watu waache kufanya kazi ili malengo yao yatimie . Klabu haipo katika mpango ambao moja kwa moja ni hasara kwa klabu kuanza kulipa fidia na kupoteza malengo yake ,"amesema Mkwasa.


Amevitaja viingilio vya mchezo huo wa kimataifa wa hatua ya mtoano wa kombe la Shirikisho Afrika kima cha chini ni 5000 , VIP B & C 20000 na VIP A ni 30000.

Mkwasa amewaomba mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuja kuishangilia timu yao siku ya Jumamosi ili kuipa sapoti timu yao pendwa.


" tunahitaji kushinda hapa nyumbani ili kupunguza ugumu wa mechi ya ugenini , hivyo sapoti yenu itakuwa ni msingi mzuri wa morali kwa vijana,"amesema Mkwasa.                       

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad