HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 22 April 2017

MBEYA: MIFUKO 400 YA SARUJI YA KUBORESHEA HOSPITALI YA RUFAA YAKABIDHIWA NA AKIBA COMMERCIAL BANK KWA RC MBEYA....


RC Makalla akikabidhiwa mifuko 400 ya saruji na Bi. Dora Saria ambaye ni Afisa Masoko wa Akiba Commercial Bank Jijini Mbeya

RC Makalla akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi na wafanyakazi wa Benki ya Akiba na Serikali kwa ujumla

Ni msaada aliouomba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla kutoka AKIBA Commercial Bank Ltd kusaidia ujenzi wa Njia za wagonjwa mita 175
Mkuu wa Mkoa amewapongeza na kuwashukuru Akiba Commercial Bank kwa namna walivyoshughulikia maombi kwa haraka 
Makalla kupitia kwa marafiki wa hospitali ya Mkoa wanaoishi ndani na nje ya Mkoa kupitia harambee wamekamilisha ujenzi wa mita 155 na awamu hii ujenzi unaendelea mita 175
ambapo jumla ya Fedha zilizotumika ni shilingi milioni 160
Ujenzi ulisimama na zinahitajika shilingi milioni 55 na ndipo tukaomba Akiba Bank.... amesema Mhe. Makalla
Kukamilika kwa ujenzi huu kutaondoa tatizo la wagonjwa kupelekwa au kwenda wodini kwa tabu kwani wakati wa mvua tatizo linakuwa kubwa 
Kwa upande wa  Akiba Commercial Bank kupitia kwa Afisa Masoko na Uendeshaji Bi Dora Saria amesema waliguswa sana Baada ya kuombwa na Mkuu wa Mkoa kutokana na wananchi kupata shida hasa wagonjwa kwenda wodini au kupeleka maiti kwenye chumba cha kuhifadhia maiti
Hivyo wameguswa na kuchangia shilingi milioni 5 sawa na Mifuko 400 ya saruji na wameaidi kutoa Mafunzo na mikopo kwa wajasiriamali 
Aidha Akiba wamevutiwa na jitihada za Mkuu wa Mkoa kuliweka jiji safi hivyo watatoa Vifaa vya usafi na kushiriki kufanya usafi mwisho wa mwezi huu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad