HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 22, 2017

CHUNYA: DC MADUSA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WAANZISHA MKAKATI KABAMBE WA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO..

Hapa Kazi Tu!! Ndivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Bi. Rehema Madusa anafanya mara baada ya yeye pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya yake kuungana kwa pamoja na kuamua kuanza kuitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya miundombinu kama barabara na majengo mengine ya kiserikali na ya kijamii kama Ujenzi wa Zahanati, Kituo cha Afya na Ujenzi wa maabara kwa shule za Sekondari. 
Katika Ziara hizo DC Madusa ameweza kubaini changamoto mbalimbali na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka ili kuwezesha gurudumu la maendeleo kusonga mbele. 
Aidha, DC Madusa akizungumza na mtandao huu amesema amejipanga kikamilifu kuhakikisha Shule za Sekondari za Wilaya hiyo zinakua za mfano kwenye mitihani kwa ngazi ya Mkoa, Kanda na Taifa kwa Ujumla, hivyo amewataka wananchi wake kumuunga mkono ikiwemo kuhakikisha Nidhamu ya wanafunzi inatazamwa kwa jicho la karibu ili kuwasaidia walimu kufanya majukumu yao pasi na matatizo yeyote
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Rehema Madusa akitoa maelekezo  kwa mfadhili kuondoa bati zisizotakiwa (G. 30) na kupaua kwa bati zenye viwango vilivyopitishwa na serikali (G. 28) katika moja ya shule huko mjini Chunya mkoani Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad