HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 22, 2017

VYETI VYA KUZALIWA SASA NI BURE KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO WA MKOA WA GEITA NA SHINYANGA

Mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano umezinduliwa rasmi tarehe 21 machi 2017 katika viwanja vya Kalangalala Geita ambapo mikoa miwili yaani Geita Mwenyeji na Mkoa wa Shinyanga kwa pamoja ulizindua mpango huo katika viwanja hivyo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi hapo jana Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe amesema kwa sasa Serikali ina dhamira ya dhati kuhakikisha kila mtoto atakayezaliwa na wale wenye umri chini ya miaka mitano watapatiwa vyeti vya kuzaliwa bure kama ilivyo elimu na chanjo na hivyo kusaidia upatikanaji wa takwimu sahii kwa ajili ya mipango mbalimbali ya maendeleo ya Nchi kwa mfano Serikali itajua kwa usahihi watoto wanaotakiwa kuanza darasa la kwanza pamoja na huduma za afya,"hivyo ndugu zangu wananchi wa Geita na Shinyanga jambo hili ni muhimu sana kwa ajili ya watoto wenu wasije kupata usumbufu hapo baadaye watakapo anza darasa la kwanza kwani wataulizwa vyeti vya kuzaliwa pia bima ya afya na baadaye elimu ya juu na ajira ni lazima vyeti vya kuzaliwa."

Mpango huu unaratibiwa na RITA kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wa kimataifa na kutekelezwa kupitia Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa ukiwa na lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi kwanai usajili unafanyika katika vituo vya tiba vinavyotoa huduma ya Mama na Mtoto pamoja na ofisi za watendaji wa kata nkatika halmashauri zote za Mkoa wa Geita na Shinyanga.

Matarajio yetu ni kusajili watoto wenye umri huo wapatao laki sita (600,000) kwa mikoa yote miwili kwani tunategemea wazazi wengi watajitokeza kutokana na wepesi wa upatikanaji wa huduma hii na hakutakuwa na malipo yoyote CHETI NI BURE, na pia urahisi wa upatikanaji wa taarifa mara baada ya mtoto kusajiliwa taarifa zake zitatumwa kwa njia ya simu maalum ya mkononi hadi kwenye kanzi data ya RITA makao makuu na mzazi atapatiwa cheti hicho papo hapo.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe(MB) akiongea na wananchi alipozindua Mpango wa kusajili na Kutoa vyeti vya Kuzaliwa bure kwa Watoto Walio na Umri chini ya Miaka Mitano unaoanza kutekelezwa katika Mikoa ya Geita na Shinyanga. Uzinduzi ulifanyika katika Kiwanja cha Kalangalala Mkoani Geita.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe(MB) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mpango wa usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa Mkoa wa Geita na Shinyanga. Wengine katika picha mbele ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga (Kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainabu Telack.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe(MB) akiwaonesha vyeti vitakavyotumika katika Mpango uliozinduliwa wa Usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa Mkoa wa Geita na Shinyanga.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe(MB) akionesha Cheti cha mtoto aliyembeba ambaye amesajiliwa katika siku ya kwanza ya Uzinduzi wa Mpango wa Kusajili na Kutoa Vyeti vya Kuzaliwa kwa Watoto walio na umri chini ya Miaka Mitano katika Mikoa ya Geita na Shinyanga.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt Harrison Mwakyembe(MB) akiwa katika picha ya kumbukumbu mara baada ya kuzindua Mpango wa Usajili wa Watoto wenye Umri chini ya Miaka mitano. Waliokaa kuanzia kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Rita, Bi Emmy Hudson, Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya RITA, Bi Victoria Lembeli, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe Zainabu Telack, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita Mhe. Joseph Musukuma na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Helman Kapufi. Waliosimama ni wafanyakazi wa RITA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad