HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 17 March 2017

VIONGOZI WA ZFA UNGUJA WAWAPONGEZA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CAFNa Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Chama cha mpira wa miguu Zanzibar (ZFA) wilaya ya Magharibi A Unguja kimewapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa uamuzi wao wa kukubali ombi la chama hicho kuwa mwanachama wa 55 wa shirikisho hilo.

Mwenyekiti wa ZFA wilaya hiyo Kheri Adam Aliy ameitaja hatua hiyo kuwa ni mafanikio makubwa katika historia ya soka la Zanzibar na Tanzania mwa ujumla.

Katika taarifa yake mara baada ya kupokea taarifa za kupatiwa uwanachama kamili kwa Zanzibar, Adam aliwapongeza pia viongozi wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Chama cha soka Zanzibar ZFA, serikali zote mbili (Zanzibar na jamhuri ya muungano wa Tanzania) kwa kuendelea kufuatia haki hiyo toka lilipowasilishwa ombi hilo mwaka 2004 na kupelekea mwaka 2006 kupatiwa uanachama mshiriki.

Aliitaja hatua hiyo iliongeza matumaini na subra kwa wadau wa Soka la Zanzibar, subira ambayo imezaa matunda baada ya sehemu hiyo ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mwanachama wa kamili.

Adam aliwataka wadau wa soka kuongeza mashirikiano kati yao na kuwasaidia viongozi wa chama cha soka wa ngazi zote kuweza kusimamia shughuli za mpira kama inavyotakiwa na CAF na mashirikisho mengine ya kimataifa.

Amesema ipo haja kwa viongozi wa wilaya kujiandaa kisaikolojia na kupokea mabadiliko mbali mbali ya uongozi na utendaji ili kuendana na matakwa ya shirikizho hilo linalosimamia masuala ya soka barani.

Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo alimpongeza Ahmad Ahmad kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa CAF akichukua nafasi ya  Issa Hayatou ambae amelitumikia shirikisho hilo kwa muda mrefu kwa kipindi cha miaka 29.
Waziri wa michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma akiwa ameshikilia bendera ya Tanzania mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Shirikisho la soka wa Barani Afrika na kuipitisha Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa 55.

Waziri wa michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma (pili kulia) akiwa na viongozi wa ZFA mara baada ya Zanzibar kutangazwa kuwa mwanachama wa 55 wa CAF.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad