HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 17, 2017

BALOZI LUPEMBE AIPA MKONO WA BARAKA AZAM KWENYE MECHI YA MARUDIANO J'PILi

BALOZI wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe, ameweka wazi kuwa Azam FC ni moja ya timu zinazowatia moyo  Watanzania wanoishi nje ya nchi, huku akiipa mkono wa ushindi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane Swallows ya Afrika Kusini.


Lupembe alitoa kauli hiyo wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

“Kwa kweli nimefarijika sana kwa kuiona Azam FC tena kama nakumbuka mlikuja hapa mwaka jana, mlikuja hapa kucheza na  Bidvest nikawa mgeni rasmi na mkono wangu ukawa wa kheri mkashinda, nawahakikishieni nitawashika tena mkono na ninauhakika mtashinda tena,” alisema Lupembe



Alisema kuwa atakuwa pamoja na timu hiyo kwa kipindi chote itakapokuwa jijini hapa hadi Jumamosi itakapoelekea Swaziland huku akiitakia kila la kheri kuelekea mtanange huo unaosubiriwa na mashabiki wengi wa timu hizo.

“Ndio tunafahamu kuwa kuna timu kubwa za Simba na Yanga, lakini Azam FC inatia moyo kwa sisi watu ambao tulioko nje nawatakia kila la kheri, mazoezi mema mimi nipo hapa kama balozi, na nitahakikisha nitakuwa na nyie mpaka siku mtakapoenda kucheza mpira,” alisema,

Lupembe aliitembelea Azam FC jioni wakati ikielekea kwenye mazoezi kujiandaa na mchezo huo.
Mara mwisho Balozi huyo kuishika mkono Azam FC iliichapa Bidvest Wits mabao 3-0 jijini Johannesburg katika mchezo wa raundi kama hii, ambapo kutokana na ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza kwa sasa timu hiyo inahitaji ushindi wowote au sare ili iweze kusonga mbele.

Balozi  wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Richard Lupembe akiwa pamoja na wachezaji wa Azam wakati alipoitembelea timu hiyo jana kwenye kambi yake katika Hoteli ya Acardia jijini Pretoria, nchini humo ikijiandaa na mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika Uwanja wa Taifa wa Somhlolo nchini Swaziland Jumapili hii saa 10.30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.alip

Kocha wa Azam ... akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mazoezi  ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.
Beki wa Kulia wa Azam, Shomari Kapombe akiwa anagombania mpira na Kingue wakati wa mazoezi ya timu hiyo  kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku  ya Jumapili.
Kiungo wa timu ya Azam, Frank Domayo (kushoto) akijaribu kumtoka mchezaji mwenzake wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku  ya Jumapili.
Nahodha wa timu ya Azam Himid Mao akijaribu kuutuliza mpira ulipigwa kwake wakati wa kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya  Jumapili.
Ramadhani Singano akiwa anapambana na Shomari Kapombe wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Mbabane Swallows siku ya Jumapili.

Makipa wa timu ya Azam wakiwa katika mazoezi.
Wachezaji wa Azam wakiwa katika mazoezi ya mwisho ya kuelekea mechi yao ya marudiano dhidi ya Mbabane Swalllows itakayofanyika Jumapili nchini Swaziland.Picha na Abducado Emmanuel.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad