Marehemu Sir George Kahama enzi za uhai wake.
MAZISHI
ya aliyekuwa Waziri na Mwanasiasa Mkongwe hapa nchini, Hayati Sir George Kahama
yanatarajiwa kufanyika kesho kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
mwili wa marehemu uliwasili nyumbani
kwake eneo la Mikocheni B kituo cha mabasi kijulikanacho kama Business
leo majira ya saa 11 jioni na kufuatiwa na shughuli ibada na kukesha hadi asubuhi.
Kesho
mwili wa marehemu utaondolewa nyumbani kwake kuelekea Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) kuanzia saa mbili
kamili kwa ajili ya viongozi mbalimbali na wananchi kutoa heshima zao za
mwisho kabla ya kuelekea Kanisa la Mtakatifu Petro ( St. Peters)
Oysterbay Dar es salaam saa tano nanusu 5.30 asubuhi kwa ibada.
Ibada ya mazishi itafanyika katika makaburi ya Kinondoni kuanzia saa tisa na nusu 9.30 alasiri.
Spika Mstaafu, Anne Makinda akisaini katika kitabu cha maombolezo cha Sir George Kahama nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.
Spika Mstaafu, Anne Makinda akimfariji mjane wa marehemu Janeth Kahama.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sofia Simba akimpa pole mjane wa marehemu, Janeth Kahama.
Mke wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Regina Lowassa (wa pili kulia), akiwa kwenye msiba huo.
Sophia Simba akisalimiana na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu katika msiba huo.
Pole zikiendelea kutolewa kwa mjane wa marehemu.
Waombolezaji wakiwa msibani.
Na Dotto Mwaibale.
No comments:
Post a Comment