HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2017

NAIBU WAZIRI MAMBO YA NDANI AFUNGUA MKUTANO WA SADC WA KUJADILI MASUALA YA USALAMA

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto meza kuu) akizungumza na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga, na kulia ni Afisa wa kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Rokhayatou Diarra.
Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wapili kulia meza kuu) akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam. Watatu kulia meza kuu ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye pia alifungua mkutano huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisindikizwa na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto), pamoja na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (kulia), mara baada ya Masauni kufungua Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo ambapo Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo walijadili masuala mbalimbali ya usalama. Warsha hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad