HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2017

LORI LAPIGA MWELEKA NA KUUA MMOJA WILAYANI MAKETE

 
Makete: Lori aina ya Isuzu TX lenye namba za usajili T 721 BVV lililokuwa limebeba mawe likiwa limepinduka katika kijiji cha Masisiwe na kusababisha majeruhi na kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa katika lori hilo

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema kuwa lori hilo lilipoteza muelekeo ghafla kisha likaanza kupinduka kwa kubiringika mara kadhaa umbali unaokadiriwa kuwa zaidi ya mita 80 kutoka barabarani

Ajali hiyo inadaiwa kutokea kati ya saa nane na saa tisa alasiri hii leo

Baadhi ya mashuhuda waliokuwa eneo la tukio ambao hawakutaka kutaja majina yao wamesema Lori hilo lilikuwa limetoka kubeba mawe kwa ajili ya kujenga daraja katika kata ya Ipepo na likiwa njiani kueleka eneo la ujenzi lilipopoteza muwelekeo na kupinduka kisha kuporomokea bondeni

Jeshi la polisi Makete lilifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi

Tutawaletea taarifa kamili ya tukio hilo pindi mamlaka husika zitakapatia.habari/picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog

Polisi wakipima jinsi ajali hiyo ilivyotokea.

Askari Polisi akiangalia mawe yaliyokuwa yamebebwa na lori hilo kabla ya kutokea ajali

Sehemu ya mashuhuda wa ajali hiyo.

Askari Polisi akijadiliana jambo na wananchi.


Mwili wa marehemu ukiingizwa kwenye gari
Lori hilo likionekana kwa mbali baada ya ajali


Muonekano wa lori hilo baada ya ajali.





Ajali ilipoanzia, hapa ndipo lori hilo lilipotumbukia



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad