HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 6, 2017

SIMBA KUCHEZA YA KIRAFIKI NA POLIS DODOMA WIKIENDI HII

SIMBA SPORTS CLUB 
Dar es salaam, Tanzania 
6/3/2017. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara, Klabu ya Simba  imekubali mwaliko wa Chama cha mpira wa miguu mkoani Dodoma (DOREFA) Kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Polisi ya mjini humo siku ya Jumamosi hii tarehe 11-3-2017. 

Kwa kuwa klabu yetu haitakuwa na mchezo wa ligi kuu wikiendi ijayo, tunaamini washabiki wetu wa Dodoma na  mikoa ya jirani watapata fursa adhimu ya kuiona ya klabu yao. Pia tunatarajia kuutumia mchezo huo Kama maandalizi ya mechi yetu ya Kombe la Shirikisho hatua ya Robo fainali itakaochezwa machi 18.

 Tunaamini pia buradani hiyo  MUBASHARA, wataipata pia watumishi wa umma ambao wameshaanza kuhamia Makao makuu ya nchi kutekeleza agizo la Mh Rais wa Jamhuri Dr John Pombe Magufuli


 Imetolewa na 

HAJI S MANARA 
MKUU WA HABARI NA MAWASILIANO SIMBA SC. 

SIMBA NGUVU MOJA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad