HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 6 March 2017

MSANII WA FILAMU KUTOKA NIGERIA AWASILI NCHINI, KUFANYA FILAMU MOJA NA WASINII WA BONGO

Msanii maarufu wa filamu kutoka nchini Nigeria, Mike  Ezuruonye amewasili nchini kwa ziara ya kikazi kwa wiki mbili kwa ajili ya kutengeneza filamu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa kampuni ya Project and Design, Halima Yahaya maarufu kama Davina amesema kuwa msanii huyo yupo nchini na atafanya filamu maalum ambayo itafanywa kwa zaidi ya wiki mbili hapa nchini.

Hata hivyo  Mike amesema yeye anajitambulisha kama msanii wa Afrika na sio Nigeria ili aweze kuwa na wigo wa kufanya kazi na msanii yoyote katika bara ili ndio maana ameona Tanzania kuna wasanii wazuri na wamemuomba kuja kufanya kazi hapa nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza na msanii maharufu filamu kutoka nchini Nigeria, Mike  Ezuruonye mara baada ya kuwasili katika ofisi ya wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam wakati alimtambulisha mmoja wa wasanii nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria, Mike  Ezuronye (kushoto) alietembelea nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa kampuni ya  Entertaiment Project and Design (EPD), Halima Yahaya almaarufu kwa jina la kisanii Davina akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam, kuhusiana na ujio wa Msanii nguli wa Filamu kutoka nchini Nigeria, Mike  Ezuronye.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad