HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 6 March 2017

JUKWAA LA KIUCHUMI LA KIFALME NCHINI KUANZA KESHO JIJINI DAR ES SALAAM

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Jukwaa la kiuchumi la kifalme lililokuwa na malengo ya kutoa elimu kwa wananchi namna ya kutafuta na kuhifadhi fedha kwa ajili ya kujiinua kiuchumi linatarajiwa kuanza kesho katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.

Mkutano huo utakaohudhuriwa na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston kutoka Marekani utakuwa ni wa siku tatu na atakuwa akitoa mada ya namna ya wafanyabiashara pamoja na wananchi wengine kujua namna ya kutafuta mtaji na kujiendeleza kiuchumi pamoja na
makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili 
.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu mkuu wa Katibu Mkuu wa taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT), Dk. Charles Sokile amesema kuw amkutano huu utakuwa na faida kubwa sana kwa wafanyabiahsra na wananchi wengine kwani kutakuwa na faida kubwa kwani kutakuwa na wafanyabiashara mbalimbali kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mbali na hilo, kutakuwa na mafunzo ya namna ya kutafuta mtaji na kujiendeleza, uadilifu wa kumpendeza mungu, serikali na kulipa kodi kwa wakati.

Sokile amesema kuwa, pia kutakuwa na maombi kwa ajili ya taifa yatakayoendeshwa na Bill Winston pamoja na aliyewahi kuwa makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili pamoja na Bishop Bernard Nwaka kutoka Zambia.
Mchungaji maarufu, mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston (wa pili kulia), kutoka Marekani akiwasili katika Hotel ya Hyatt KIlimanjaro Dar es Salaam leo ambapo atatoa mada katika Mkutano Mkubwa wa Kiuchumi wa siku tatu pamoja na Maombi ya Kitaifa 2017 unaotarajiwa kuanza jijini humo kesho. Mkutano huo unaandaliwa na taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT). Pamoja naye kutoka kushoto ni, Mkurugenzi Mtendaji wa KLNT, Isaac Mpatwa, Mratibu wa Kamati ya Maandalizi, Carol Mbaga na Katibu Mkuu wa KLNT, Dk. Charles Sokile
Katibu Mkuu wa taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT), Dk. Charles Sokile akizungumza na waandishi wa habari juu ya mkutano mkuu wa jukwaa la kiuchumi unaootarajiwa kuanza kesho. Kulia ni mwanasheria wa KLNT Fred Ringo.

Mwenuyekiti wa bodi ya wadhamini wa Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT) Bishop Bernard Nwaka (katikati) akijadiliana jambo na ni mwanasheria wa KLNT Fred Ringo (kulia) na Katibu Mkuu wa KLNT, Dk. Charles Sokile.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad