Mtaa Kwa Mtaa Blog

MATUKIO KATIKA PICHA: MECHI YA RUVU SHOOTING NA YANGA UWANJA WA TAIFA LEO

Timu ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu Tanzana Bara uliopigwa leo katika Uwanja wa Taifa.

Magoli ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva kwa njia ya penati katika dakika ya 31 baada ya mchezaji wa Ruvu kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari na Emanuel Martin akimalizia pasi safi ya Msuva kwenye dakika ya 90.

Katika dakika ya 45, Obrey Chirwa anapewa kadi ya nyekundu kwa makosa mawili baada ya mwamuzi kusema ameunawa mpira kabla ya kufunga na baadae kufanya utovu.

Dakika 45 za kipindi cha pili, Yanga waliendelea kusaka goli la ushindi huku Ruvu shooting wakiwa wanatafuta la kusawazisha ambapo mpaka dakika 90 matokeo ni Yanga 2-0 Ruvu Shooting.

Baada ya matokeo haya Yanga wanaendelea kusalia katila nafasi ya pili wakiwa na alama 52 wakiwa nyuma ya Simba wenye alama 54.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget