HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 1, 2017

OPERESHENI YA VIROBA YAFUMANIA KIWANDA CHA NYATI SPRIT KUWA VIROBA

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Utekelezaji wa opesheni hiyo umeanza kufanyika leo  baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,  Muungano na Mazingira,  January Makamba alipotangaza marufuku hiyo Februari 20  juu ya vileo vilivyo katika vifungashio viondoke katika mzunguko wa biashara  na watengenezaji wahamie katika mfumo wa chupa kwa kuanzia milimita 250.
 Operesheni ya kukamata viroba imeanza leo  jijini Dar es Salaam ikisimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais  Katika Kiwanda cha Kampun ya nyati spirit kilichopo Vingunguti ambapo  katoni za viroba 7067  aina ya nyati  zimekutwa katika kiwanda hicho.
Akizungumza katika operesheni Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na Chakula  (TFDA ), Emmanuel Alphonce amesema operesheni imeanzia jiji la Dar es Salaam na kesho itaendelea nchi nzima chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mikoa
 Mkurugenzi wa kiwanda hicho Rupa Suchik amesema hatatengeneza tena viroba ikiwa ni agizo la serikali na vilivyopo watateketeza .              
Amesema  kuanzia jana ameshapunguza wafanyakazi 150 kutoka 300  kutokana na agizo hilo na hao wataingia katika mfumo wa uzalishaji vileo katika mfumo wa Chupa.
 Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na Chakula  (TFDA ), Emmanuel Alphonce akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya operesheni ya viroba katika kiwanda cha nyati sprit leo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
 Vijana wakipanga Viroba katika boksi walipokutwa na timu ya operesheni viroba iliyofika katika kiwanda cha Nyati Sprit leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Sehemu ya Katoni za Viroba vilivyokutwa katika kiwanda cha nyati sprit leo jijini Dar es Salaam.
Mafisa wa serikali wakikagua nyaraka mbalimbali za kiwanda cha Nyati Sprit ikiwa ni uhalali wake wa kuendelea kufanya biashara katika mfumo mpya kutoendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad