HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 1, 2017

IFC yafanya uzinduzi wa kampeni ya kukuza uelewa kwa watumiaji wa simu, kutuma na kupokea pesa moja kwa moja kutoka mitandao yote

Taasisi tanzu ya Benki ya Dunia, IFC imezindua kampeni ya Huduma ya kutumia fedha kwenda mtandao wowote bila garama.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa kutoka  Benki Kuu Tanzania,  Bernard Dadi amesema   huduma hiyo mpya itawanufaisha  wananchi kupunguza garama za kutumia fedha kwenda mitandao mingine.

Amesema kuwa kampeni hiyo itaongeza uelewa wa watumiaji simu za mkononi nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila garama.
"Uwezekano huu wa huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenda kwenye akaunti ya mtumiaji, unatarajiwa kuongeza idadi ya watu wanaofaidika na huduma za kifedha nchini", amesema Dafi

Amesema kuwa kufanikiwa kwa Huduma hii ambayo kampeni yake ina lengo la kufikia watu milioni moja katika kipindi cha miezi sita kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya Kwanza duniani ambako makampuni ya simu yamekubaliana  na wateja wao kutumiana fedha moja kwa moja.
Kampeni hiyo inayoongozwa na FEM Tanzania Ltd,  inafanikishwa kwa msaada wa BOT, Taasisi ya Bill & Gates na Shirika la the Financial Sector Deepening.
Amesema, uchunguzi iliofanywa na IFC imebaini ukosefu wa uelewa wa Huduma hiyo miongoni mwa watumiaji kwa kukosa kuaminiana miongoni mwa makampuni ya simu na ushindani kwenye masoko.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, BOT, Bernard Dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari,hawapo pichani juu ya Huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote bila garama.
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo y Taifa, BOT Bernard Dadi wa nne kutoka kushoto na wadau mbali mbali wa kampuni za simu nchini, wakiangalia onyesho la uzinduzi kutoka kwa Vijana wanaofanya kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Huduma ya kutuma fedha kwenda mitandao yote.
 Mkurugenzi Bernard Dadi wa pili kulia, Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedun na wadau wengine mbali mbali kutoka katika makampuni ya simu wakifuatilia kampeni za uzinduzi wa Huduma za fedha kwa njia ya simu bila garama yoyote. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad