HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 7 March 2017

DCB YATOLEA UFAFANUZI MAKUBALIANO YAO NA MANISPAA YA KINONDONI

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari wakati akitolea ufafanuzi juu ya makubaliano baina yao na Manispaa ya Kinondoni. Kushoto ni Meneja uendeshaji wa Matawi DCB Haika Machaku.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BENKI ya DCB imetolea ufafanuzi makubaliano yao na manispaa ya Kinondoni kuhusiana na mikopo ya vijana na wanawake iliyokuwa ikitolewa na benki hiyo ambapo kwa sasa imesitishwa kwa muda.

DCB wamesema kuwa katika gazeti la Uhuru la tarehe 2 machi lilimnukuu  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi kuwa mfumo wa benki hiyo unaotumika kuwakopesha vijana na wanawake kuwa kuna mazingira yasiyo rafiki na kusababisha vijana wengi kupata mikopo hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa amesema kuwa, taarifa hiyo haina ukweli wowote kwani wao waliingia makubaliano ya kimaandishi na Manispaa ya Kinondoni ya kuwapatia mikopo vijana na wanawake na wamekuwa wanafanya hivyo na wamekuwa wanatoa mikopo kwa bei nafuu ingawa Desemba 13, 2016 walipokea barua ya kusitisha kutoa mikopo hiyo kutokana na kuwa na mgawanyiko wa Wilaya ya Kinondoni.

Mkwawa amesema, taarifa zilizoandikwa na gazeti hilo si za kweli kwani wao walikuwa wanatoa mikopo kwa vijana na toka waingie makubaliano hayo wameshapokea fedha takribani bilioni mbili na wamefanikiwa kukopesha vijana na wanawake wa wilaya hiyo.

"Hata ukienda  DCB Commercial Bank ukiwaambia  wakupe mrejesho wa fedha walizozichukua za halamashauri kwa ajili ya kukopesha hawana na kwamba fedha hizo inafanyia biashara kinyume na lengo la Manispaa ya Kinondoni la kutoa mikopo hiyo bila riba"gazeti la uhuru lilimnukuu Mkuu wa Wilaya Kinondoni.

Mkwawa amesema kuwa kwa sasa wamemtumia barua Mkuu wa Wilaya Kinondoni barua ya kukanusha taarifa hiyo kwani benki ya DCB ilikuwa inatoa mkopo huo kwa wananchi bila masharti magumu pia barua kwa gazeti la Uhuru.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad