HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 7, 2017

VIGOGO WATANO WAHOJIWA KWA TUHUMA ZA MADAWA YA KULEVYA

 
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumkabidhi orodha ya majina 97 Kamishna wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, sasa orodha hiyo imeanza kufanyiwa kazi kwakuwa vigogo watano waliopo kwenye orodha hiyo wameanza kuhojiwa.

Kamishna wa Intelijensia wa Mamlaka hiyo, Fredrick Kibula alisema Jumatatu hii kuwa wanawahoji na wanafanya uchunguzi dhidi ya watuhumiwa hao kabla ya kuwafikisha katika Mahakama.
Alisema, “Tuna watu muhimu watano wanaotoka katika orodha ile ya mkuu wa mkoa. Tunao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na muda ukifika tutawatajia mtawafahamu. “Hatukamati ovyo ovyo ni lazima tujiridhishe bila shaka kwamba wahusika wana sifa ya kukamatwa. Pia hatutangazi ingawa tunafanya operesheni za kiuchunguzi ambazo zinafanyika mara kwa mara.”
Tarehe 13, Februari wwaka huu,RC Makonda alimkabidhi Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Rogers Sianga orodha ya majina 97 awamu ya tatu ya watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad