HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 24 February 2017

WAZIRI MWIJAGE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KIWANDA KIPYA YA VIGAE CHALINZE

Viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za Uzinduzi wa Uwekaji wa jiwe la msingi wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi huo. Sherehe za Uzinduzi huo zilifanyika eneo la mradi huko Chalinze.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage akihutubia wageni waliohudhuria Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Kiwanda cha Twyford Ceramic Tiles. Mh. Mwijage alisema Viwanda Vikubwa ambavyo vitatoa ajira na kuongeza pato la taifa vitajengwa na Watanzania watarajie mengi zaidi katika utekelezaji wa Agenda ya viwanda ii kuleta maendeleo kwa Taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Evarist Ndikilo akitoa machache wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha Twyford Ceramics Tyles na kusisitiza anayependa kushuhudia ujenzi wa viwanda atembelee Mkoa wa Pwani kwani hapo ndiyo mahala ujenzi wa viwanda vingi unapofanyika.
Picha ikionyesha wananchi wa Chalinze waliofika kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramic Tiles. Wananchi hao waliongozwa na Mbunge wao wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.
Picha ya pamoja ikimuonyesha Ndugu Clifford Tandari Kaimu Mkurugezni wa Kituo cha Uwekezaji, Ndugu Majjid Mwanga, Mkuu wa Wilaya ya Chalinze, Mh. Evarist Ndikilo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, MhCharles Mwijage, Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji, Ndugu Jacq Feng Mkurugenzi wa Kiwanda cha Twyford Ceramic Tiles, Mh Ridwani Kikwete Mbunge wa Chalinze kwenye sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi. Nyuma ni taswira ya jinsi ambavyo kiwanda kitakavyokuwa mara baada ya ujenzi kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad