HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 24, 2017

Lowassa kuudhuria mechi ya Simba na Yanga Taifa kesho

Waziri mkuu wa Zamani na Mjumbe wa kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa kesho atakuwa miongoni mwa maelfu ya washabiki watakaoudhuria pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kwenye dimba la Taifa jijini dars es salaam.

"Kesho nakwenda uwanjani, usitake kujua mimi ni mshabiki wa timu gani, subiri utaniona  uwanjani" amesema Lowassa ambaye hajawai kuweka wazi ni mshabiki wa timu gani, zaidi ya kusema anaipenda Manchester United.

Lowassa amesema kinachomsukuma zaidi kwenda uwanjani ni kuungana na Wadau  wa soka nchini kutaka kuiona ligi ya mpira Tanzania inakuwa na msisimko kama ile ya ligi za nje.

"nasikitika napoona watu tunazipenda sana timu za nje..Yale mahaba ya zamani kwa timu zetu yako wapi? michezo hususani mpira ni eneo pana sana la ajira kwa vijana wetu" alisema Lowassa ambaye alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wa kikapu hapo zamani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad