HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 24 February 2017

WANASHERIA WAASWA KUWASAIDIA WANYONGE ZAIDI NA KUAACHA KUWASAIDIA WAHALIFU- MAKONDA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  amewataka wanasheria wa mkoa wa Dar es Salaam  kujitoa kwa kuwasaidia wanyonge na masikini kuweza kupata haki zao na sio kutumia taaluma katika  kuwatetea watu wanaofanya uhalifu.
Makonda  ameyasema hayo wakati alipokuwa akipokea mrejesho kwa wanasheria waliojitolea kutoa msaada wa kisheria kwa jiji la Dar es Salaam, amesema kuwa kuna watu wanakosa haki kutokana na kukosa msaada wa kisheria.
Amesema kuwa wanasheria wa mkoa wa Dar es Salaam wakijitoa watakuwa wamesaidia wananchi kupata haki pamoja na kupunguza migogoro iliyopo.
Makonda amesema vijana waliotoa msaada  wa kisheria wameonyesha uzalendo na kuwataka kuendelea kuwatumikia wananchi.
Mwakilishi wa Wanasheria waliojitolea  kutoa msaada wa Kisheria, Georgia  Kamina amesema kuwa wamesaidia makundi mengi ikiwa ni pamoja na kukutana na wananchi.
Georgia amesema walichojifunza katika kazi walioifanya  ni wananchi kushindwa kujua sheria na jinsi ya kupata haki.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu umuhimu wanasheria kujitoa kwa ajili ya kuwatetea wanyonge leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwakilishi wa Wanasheria waliojitolea  kutoa msaada wa Kisheria, Georgia  Kamina.Picha na Emmanuel Massaka,Globu yaj  jami.
 Mwakilishi wa Wanasheria waliojitolea  kutoa msaada wa Kisheria, Georgia  Kamina akizungumza na waandishi wa habari juu msaada wa sheria walitoa kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
 Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad