HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 17, 2017

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE”

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu. Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-

KUKAMATA WATUHUMIWA WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA UUZAJI/USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako katika maeneo ya Manga na Nsalaga – Uyole na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na wauzaji, wasambazaji na watumiaji [mateja]. Watuhumiwa waliokamatwa kutokana na kujihusisha ba usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao ni 1. SHABAN RAMADHAN [40] Mkazi wa Uyole 2. RASHID YASIN [35] Mkazi wa Nonde 3. RODA MWAMBERA [60] Mkazi wa Mama John 4. MRISHO RAMADHAN [22] Mkazi wa Airport - Iyela na 5. MUSSA KIMBE [33] Mkazi wa Nonde.

Watuhumiwa wote wapo mahabusu na mahojiano zaidi yanaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.

KUKAMATA WAUZAJI/WASAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA.

Aidha kufuatia misako iliyofanyika kuanzia tarehe 19.01.2017 hadi tarehe 09.02.2017 katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya, Watuhumiwa wawili walikamatwa katika matukio mawili tofauti wakiwa na dawa za kulevya.

Katika msako wa kwanza uliofanyika maeneo ya Ilemi Jijini Mbeya, HENRY MWAMFUPE [19] Mkodishaji Baiskeli na Mkazi wa Ilemi alikamatwa akiwa na kete 03 za dawa za kulevya aina ya Heroine.


Pia katika msako uliofanyika maeneo ya Mbalizi, ANITHA ABEL [21] Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Sanani iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na Mkazi wa Mbalizi alikamatwa akiwa na kete 15 za dawa za kulevya aina ya Heroine akiwa nyumbani kwao.

Mtuhumiwa anaishi na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la MARTHA MWALINDU ambaye alikimbia baada ya kuwaona askari na inasadikika ndiye muuzaji/msambazaji mkubwa wa dawa hizo za kulevya na huwa anamtumia mtoto wake kuuza na kusambaza. Msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea.

Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya Upelelezi kukamilika.

KUKAMATA WATUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA [MATEJA].

Aidha katika misako mbalimbali iliyofanyika walikamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya maarufu kama Mateja ambao ni:-
         AYUBU ABDALLAH [42] Mkazi wa Ilomba jijini Mbeya
         EMANUEL SIMBEI [43] Mkazi wa Sokomatola
         IMAN ABBAS [33] Mkazi wa Majengo
         SHABAN SHAIBU [19] Mkazi wa Nonde
         KENY SANGA Mkazi wa Sokomatola
         PASCHAL PIUS [28] Mkazi wa Itiji
         PILIM KAYANGE [20] Mkazi wa Uhindini
         ELISHA MWAIHABI [19] Mkazi wa Nonde
Wengine ni:-
         DANIEL KANJANJA [43] Mkazi wa Uhindini
         MUSSA KIPESA [37] Mkazi wa Iwambi
         CHARLES GERVAS [28] Mkazi wa Nonde
         KIMANZI KILONZA [44] Mama John
         SHABAN SHAIBU [26] Mkazi wa Nonde
         EMANUEL LUCAS [18] Mkazi wa Ilomba
         RICHARD GONDWE [40] Mkazi wa Ivumwe
         HENRY LEMA [35] Mkazi wa Mama John
         RAMADHAN ABBAS [18] Mkazi wa Sae
         EDWARD MWASEKA [30] Mkazi wa Majengo
         LUSEKELO KIDION [26] Mkazi wa Mwakibete
         ALINANUSWE STIVEN [26] Mkazi wa Ilolo
         JUSTIN WISTON [23] Mkazi wa Mafiati
         MICHAEL KASHILILIKA [20] Mkazi wa Manga
         KANI ASANGALWISYE [28] Mkazi wa Ituha.
Watuhumiwa wapo mahabusu wanaendelea kuhojiwa ili kupata mtandao halisi wa wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya.

KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA [BHANGI].

Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya. Katika misako hiyo iliyofanyika maeneo ya Mabatini na Ilomba jijini Mbeya, watuhumiwa wanne walikamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya Bhangi misokoto mitatu yenye uzito wa gram 15.

Watuhumiwa waliokamatwa ni 1. GEOFREY ADAMSON [35] Mkazi wa Mabatini 2. ZUBER MWAMBENYA [24] 3. GWAKISA ANYOSISYE [20] wote wakazi wa Mama John na 4. PHILIBERT MOSES [35] Mkazi wa Nonde.

KUPATIKANA NA MICHE YA BHANGI.

Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya kuanzia saa 17:00 hadi saa 17:45 jioni msako ulifanyika maeneo ya Soweto Mtaa wa Mkombozi, Kata ya Ruanda na maeneo ya Nonde, Kata ya Nonde, Tarafa ya Sisimba, Jiji na Mkoa wa Mbeya na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na miche ya Bhangi 18 na mbegu zake.

Watuhumiwa hao ni 1. DENIS DAVID [30] Mkazi wa Soweto ambaye alikamatwa akiwa dukani kwake na 2. STIVIN VENANCE [18] Mkazi wa Nonde. Upelelezi unaendelea.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na mahojiano na watuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa watu wanaojihusisha nao katika biashara ya dawa za kulevya.

KUPATIKANA NA POMBE MOSHI [GONGO]

Mnamo tarehe 10.02.2017 majira ya saa 21:00 usiku katika msako uliofanyika huko maeneo ya Mafiati, Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya watuhumiwa wawili walikamatwa wakiwa na Pombe Moshi ujazo wa lita 10.

Watuhumiwa hao ni 1. FRANCIS NDEZI [32] Mkazi wa Forest na 2. JAMES KAJANJA [38] Mkazi wa Forest ya Zamani. Upelelezi unaendelea.


KUKAMATA WATUHUMIWA WANAJIHUSISHA NA MATUKIO YA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA NA KUTEKA MAGARI.

Mnamo tarehe 12.02.2017 kuanzia majira ya saa 20:00 hadi saa 23:45 Usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya msako huko katika vijjiji vya Mabadaga na Mpakani vilivyopo Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya jirani na barabara kuu ya Mbeya kwenda Njombe. Msako huo ulilenga kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na matukio ya unyang’anyi wa kutumia na silaha na utekaji magari wakati wa usiku.




Katika msako huo jumla ya watuhumiwa 11 wamekamatwa ambao ni 1. EMANUEL MANGA [30] Mkazi wa Njombe 2. ZAWADI MAKOGA [33] Mkazi wa Makambako 3. ISSA ABIBU [45] Mkazi wa Mbeya 4. FRICK MCHAMI [26] Mkazi wa Machimbo 5. MPAJI KAPUNGU [38] Mkazi wa Lugelele na 6. RICH KIHOMBO [25] Mkazi wa Ubaruku.

Wengine waliokamatwa ni 7. MUSSA MTWEVE [27] Mkazi wa Machimbo – Mbarali 8. WILBERT MAGAINA [36] Mkazi wa Mlomboji 9. IBRAHIMU TWEVE [35] Mkazi wa Mlomboji – Mbarali 10. JOHN MBAFO [48] Mkazi wa Machimbo na 11. ZABRON MWILONGO [20].

Aidha katika msako huo Pikipiki 4 zilikamatwa baada ya watuhumiwa kuwaona Polisi na kuzitelekeza na kukimbia. Pikipiki hizo ni yenye namba 1. MC 254 BHK aina ya Kinglion 2. MC 264 AZZ aina ya Kinglion 3. MC 521 BYC aina ya Sanlg na 4. MC 565 BGE aina ya Kinglion. Upelelezi unaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na matukio hayo.

KUKAMATA WAHAMIAJI HARAMU.

Mnamo tarehe 13.02.2017 majira ya saa 09:00 asubuhi huko Eneo na Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, wahamiaji haramu watatu wote raia na wakazi wa nchini Ethiopia walikamatwa kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Wahamiaji hao ni 1. AGAFA SHAMENO [22] 2. BEKELE SEDESO [29] na 3. SESEBE SHIFUHA [24]. Upelelezi unaendelea.

WITO:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua watu na mtandao wa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Aidha Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani inasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Imesainiwa na:
[DHAHIRI A. KIDAVASHARI - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad