Hakimu
mkazi wa Wilaya ya Chunya Desdery Magezi amemhukumu kwenda jela miaka
ishirini na viboko nane Maneno Pesambili Kanjanja au Maneno Pesambili
Lyimo(59)mkazi wa kijiji cha Kiwanja Kata ya Mbugani Wilaya ya Chunya
baada ya kumkuta na hatia ya kumwingilia kimwili binti yake mwenye umri
wa miaka 19 na kumfungia ndani kwa miaka miwili na kumnyima haki za
msingi kama chakula na kisha kumsababishia ulemavu wa miguu kwa
kushindwa kutembea.

Mwendesha
mashitaka wa Serikali Frederick Ndosi amesema kuwa kosa hilo ni kinyume
cha sheria namba 158 (1)b sura ya 16 iliyopitiwa mwaka 2002 ambapo
mshitakiwa amedaiwa kutenda kosa hilo katika vipindi tofauti kati ya
2015 hadi 23 Januari mwaka alipokamatwa na kufikishwa mahakamani januari
30 mwaka huu. Upande wa mashitaka ulileta mashahidi watano akiwemo
mtoto aliyefanyiwa ukatili na mahakama kuridhika pasipo shaka na
ushahidi wake.
Hata
hivyo Ndosi aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe
fundisho kwake na wengine wenye kufanya vitendo vivyo. Akijitetea mbele
ya Mahakama Maneno amesema kuwa kesi hiyo imetengenezwa ili kumtia
hatiani hivyo mahakama imuonee huruma kwa kuwa hakutenda kosa hilo.
Baada ya Hakimu Magezi kusikiliza pande zote mbili mbili alimtia hatiani
mshitakiwa na kumtaka kwenda jela miaka ishirini na viboko nane ili
kutengwa na jamii.
Nje
ya Mahakama binti aliyetendewa ukatili huo amesema kuwa adhabu hiyo ni
ndogo hata kama ni Mzazi wake na anajisikia vibaya anapokumbuka tukio
hilo na kuamua kubadilisha jina na sasa kuitwa Mariam Maneno.
Aidha amewashukuru wasamaria wema ambao wanaendelea kumhifadhi akiwemo mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa.
No comments:
Post a Comment