HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 15 February 2017

SERIKALI YATOA UFAFANUZI JUU YA WATANZANIA WALIOFUKUZWA MSUMBIJI

Naibu Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda,Dk Susan Kolimba

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Wizara ya mambo ye nje na ushirikiano wa kikanda ametoa ufafanuzi juu ya tatizo la watanzania waliopo Msumbiji wanaokabiliwa na changamoto ya kurudishwa nyumbani.

Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jijini Dar es Salaam leo Naibu Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda, Dk Susan Kolimba amesema kuwa amepokea taarifa za kukamatwa na kufukuzwa kwa raia wa Tanzania waliokuwa wakiishi katika mji wa Monte Puez ulio Cabo Delgado, Jamhuri ya Msumbiji.
                                        
Na kuweka wazi kuwa Serikali ya Msumbiji imekiri kuwepo kwa operesheni maalum ya kuwakamata na kuwarudisha raia wa nchi za kigeni wanaoishi katika mji huo bila kufuata Sheria za Uhamiaji za nchi hiyo. Aidha, Serikali hiyo imetaarifu kwamba, zoezi hilo limeanzia mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

“ Kufuatia hali hiyo, Ubalozi wetu nchini Msumbiji upo eneo la tukio ili kufuatilia suala hili na kujionea hali halisi. Aidha, unaendelea kufanya mawasiliano ya Kidiplomasia na Serikali ya Msumbiji ili kuhakikisha usalama wa Watanzania na mali zao. Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.

Kuanzia zoezi hilo lilipoanza, Raia wa Tanzania wapatao 132 wamesharudishwa nchini. Tarehe 11/02/2017 walirejeshwa raia 58. Tarehe 14/02/2017 wamerejeshwa raia 24 na leo tarehe 15/02/2017 wamesharejeshwa raia 50 ”amesema Naibu Waziri.

Ameongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahakikishia Watanzania kuwa uhusiano kati ya Tanzania na jirani yetu Msumbiji ni mzuri. Hivi karibuni mwezi wa Desemba 2016, Tanzania na Msumbiji zilifanya mkutano wa ujirani mwema uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Mkutano huo uliofanyika kwenye mji wa Pemba ulio Cabo Delgado uliainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo masuala ya biashara na uhamiaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad