HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 15, 2017

SERIKALI YA JAPAN YAISAIDIA TANZANIA DOLA 80,234 KUENDELEZA MCHEZO WA BASEBALL

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (aliyesimama mbele) akiongea na Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida (aliyesimama mbele kulia) akiongea na Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Baseball Tanzania (TaBSA), Dkt. Ahmed Makata (aliyekaa kushoto mbele) akisaini Mkataba wa Ujenzi wa Uwanja wa Baseball, kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaharu Yoshida.Wanaoshuhudia nyuma ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye pamoja na Mjumbe toka Japan.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (aliyesimama nyuma) akipongeza wakati ubadilishanaji wa Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati waliokaa wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan, Mhe. Masaharu Yoshida pamoja na viongozi wengine mara baada ya hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa kiwanja cha Baseball nchini kati ya Serikali ya Tanzania na Japan leo 15 Februari, 2017 Jijini Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad