HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 2 February 2017

MISRI YATINGA FAINALI AFCON, KUISUBIRIA KATI YA CAMEROON AU GHANA

Mlinda mlango mkongwe katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika na Nahodha wa Timu ya Misri, Essam El Hadary leo ameibuka kuwa nyota wa mchezo kwa kuiwezesha Timu yake kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kufanikiwa kuitoa timu ya Burkina Faso kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia dakika 120 za mchezo huo kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1. 

Kipa huyo ambaye aliweza kuicheza michomo miwili kwa ustadi kabisa, ameoneka kuendelea kuwa bora zaidi pamoja na umri wake kuwa mkubwa. Kipa huyo ambaye alichukuliwa na timu yake ya Taifa kushiriki michuoano hiyo akiwa ni kipa wa akiba, alifanikiwa kuingia langoni baada ya kipa kinda wa timu hiyo aliekuwa kwenye kikosi cha kwanza kuumia katika michezo ya awali na kulazimika mkongwe kuyo kuvaa tena "groves" na kuingia dimbani.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wenye kasi ya aina yake huku timu zote zikionyeshana uwezo wa kushambuliana kwa zamu. Misri ndio walioanza kuliona lango la wapinzani wao mnamo dakika ya 66 kupitia kwa Mshambuliaji wake, Mohamed Salah na dakika saba baadae (73) Burkina Faso walisawazisha goli kupitia kwa Aristide Bance.
Misri sasa itamsubiria mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili itakayopigwa hapo kesho kwa kuwakutanisha miamba wawili ambao ni Cameroon na Ghana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad