HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 20 February 2017

MBUNGE VITI MAALUMU IRINGA AENDELEZA ZIARA KATIKA WILAYA YA MUFINDI


MBUNGE wa Viti Maalum Iringa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Rose Tweve ameendelea na ziara zake katika Wilaya za mkoa huo ambapo mwishoni mwa wiki hii alitembelea kata ya Wambi iliyopo kwneye wilaya ya Mufindi.

Rose katika moja ya ahadi zake wakati wa kampeni aliweza kuwaahidi wanawake wa mkoa huo kuwainua kiuchumi hususani katika kuwawezesha kwa kuwapatia fedha na pia kuwashauri kujiunga na vikoba na pia kuhakikisha jumuiya za wanawake zinakuwa imara.

Akiwa katika kata ya Wambi, Rose amezungumza na wakina mama wa Jumuiya ya wanawake wa Mkoa wa Iringa (UWT) na kuwataka kujiingiza katika masuala ya ujasiriamali ili kuweza kujiinua kiuchumi hasa katika kujiunga na vikundi vya Vikoba.

Rose amewaambia kuwa, wanawake wanatakiwa kubadilika na kuacha kuwa tegemezi kwa wanaume kwani watakapojiwezesha kiuchumi wataweza kuondokana na utegemezi ambapo pamoja na hayo aliweza kuwapatia kiasi cha shilingi laki sita (600,000) kwenye jumuiya hiyo.

Wanawake wa kata ya Wambi wametakiwa kuwapa fursa sawa watoto wa kike na kiume katika suala la elimu kwani itakuwa ni moja ya fursa ya kuwawezesha kielimu.

Katika ziara hiyo, Rose aliongozana na Diwani wa kata ya Wambi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Damian Kyando ambapo katika mkutano huo na wakina mama wa kata yake aliweza kuchangia kiasi cha shilingi laki moja (100,000) na kuwataka wajishughulishe na kuachana na masuala ya utegemezi kwa wanaume.
 Mbunge wa Viti Maaalum Iringa (CCM) Rose Tweve akizungumza na wanawake wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Iringa wakati wa ziara yake endelevu ya kati ya Wambi Wilaya ya Mufindi.
  Mbunge wa Viti Maaalum Iringa (CCM) Rose Tweve akisalimiana na Mtendaji wa kata ya Wambi Veronica Masenga akiwa pamoja na Diwani wa Viti Maalum Asha Nyenza (katikati) na Diwani wa wa kata ya Wambi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Damian Kyando wakati wa ziara kwenye kata hiyo.
  Mbunge wa Viti Maaalum Iringa (CCM) Rose Tweve akikabidhi fedha kiasi cha Shilingi cha laki sita (600,000) kwa moja ya akina mama wa  wanawake wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Iringa, kulia ni Diwani wa wa kata ya Wambi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Damian Kyando ambae alishiriki kwenye ziara hiyo na wa kwanza kushoto ni Diwani wa Viti Maalum Asha Nyenza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad