HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 6, 2017

MBUNGE VITI MAALUM AIPONGEZA SERIKALI KWA KUFUNGUA VITUO VYA BENKI YA WANAWAKE MKOANI IRINGA

Mbunge wa Viti Maalum Iringa, Rose Tweve akiuliza swali bungeni.

Na Ripota wa Globu, Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum Iringa Rose Tweve ameipongeza serikali kwa kuweza kufungua vituo vya benki wa wanawake mkoani humo na kutaka kupeleka huduma hiyo kwenye maeneo mengine kwani wanawake wameamua kujiwezesha kimaisha kwa kujihusisha na ujasiriamali.


Rose alisema hayo baada ya kujibiwa swali bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla kuhusiana na kufungua kituo kwenye wilaya ya Mufindi ambapo kuna benki ya Mufindi Community Bank (MUCOBA)  kwani ni moja ya maeneo yanayokuwa kwa kasi sana ndani ya mkoa wa Iringa..



Akijibu swali hilo, Kigwangalla alisema kuwa mpaka sasa wananchi zaidi ya 6850 wameweza kupata mikopo kutoka katika benki ya wanawake ambapo zaidi ya wanawake 5350 wamechukua kutoka wilaya Makambako na Iringa Mjini lakini pia wanawake kutoka wilaya ya Mufindi wamefaidika pia.


Akifafanua zaidi kuhusiana na mpango mkakati wa serikali wa kuongeza vitu hivyo , Kigwangalla amesema kuwa kukosekana kwa mtaji wa kutosha kwenye serikali ndiyo sababu kubwa ya kushindwa kutanua vituo vya benki ya wanawake mikoa mbalimbali kwani mpaka sasa wameshafungua takribani mikoa saba nchini.

Mpaka kufika Desemba 2016 mikoa iliyoweza kupata huduma ya kituo cha benki ya wanawake ni Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Dodoma na Iringa  ambapo wamefungua vituo 252 nchini na tayari mkopo wa takribani milioni 120 zimeshapokeshwa kwa wananchi 146 wa Iringa wakiwemo wanawake 117 na wanaume 32.

Kigwangwalla alisema kuwa madirisha hayo ya mkoani Iringa yalifunguliwa mwaka 2014 ila mchakato bado unaendelea na iwapo serikali itafanikiwa kupata mtaji wataongeza vituo mkoani humo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad