Mtaa Kwa Mtaa Blog

FILAMU ZA KIBONGO KUTIKISA TUZO ZA DStv AFRICA MAGIC VIEWERS’ CHOICE 2017

Wakati filamu zitakazochuana katika tuzo za mwaka huu za Africa Magic Viewers’ Choice (AMVCAs) zikitangazwa, filamu kutoka Tanzania zimeibuka katika Makundi matatu tofauti, kitendo kinacholeta matumaini ya kuona makubwa ya watanzania kuwika kwenye tuzo hizo zitakazofanyika katika jiji la Lagos nchini Nigeria hapo mwezi Machi 2017.

Filamu za Kitanzania zinawika katika kundi la Filamu Bora kabisa Afrika Mashariki ambapo kati ya filamu tano zilizoteuliwa, tatu ni za kitanzania ambazo ni “Aisha” ya Amil Shivji, “Naomba Niseme” ya Staford Kihore, na “Homecoming” ya Seko Shamte. 
Kundi jingine ambalo filamu za Tanzania zimejitokeza ni lile la Filamu Bora za lugha ya Kiswahili ambapo tamthilia ya “Siri ya Mtungi” awamu ya pili ya John Louise na Jordan Riber imeteuliwa kushiriki Kwenye kundi kubwa la Sinema Bora barani Africa mwaka 2016, sinema mbili kati ya sita zilizomo katika kundi hilo ni za Tanzania ambazo ni “Aisha” ya Amil Shivji na “Naomba Niseme” ya Staford Kihore. 

Upigaji wa kura kupendekeza washindi unaendelea hadi februari 24 ambapo utafungwa rasmi na hafla ya kutangaza washindi itafanyika tarehe 5 Machi 2017. 

Upigaji kura unafanyika kwa njia ya mtandao na pia mpigakura anaweza kutembelea www.africamagic.tv au www.dstv.com ambapo ataweza kupelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa wa kupigia kura. 

 Akizungumzia tuzo hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, amewasihi watanzania kupiga kura kwa wingi ili kuwawezesha washiriki wetu kuibuka washindi. 

Amesema kwakuwa washiriki ni wengi na wanatoka nchi mbalimblai kote Afrika, ni uzalendo pekee wa kuwapigia kura watanzania wenzetu ndio utakaowahakikishia ushindi. 

“Sasa Ni Zamu yetu” alisema Maharage na kuongeza “Kitendo cha kazi za hawa watanzania kuingia kwenye mchuano, kinamaanisha kazi zao zina ubora unaokubalika, hivyo inabidi tuwaunge mkono kwa kuwapigia kura nyingi kadiri iwezekanavyo, Watanzania wanatambua kuwa sasa ni zamu yetu, na sisi tuuonyeshe ulimwengu kuwa tunaweza” alisema. 

Tanzania ina rikodi nzuri kwenye tuzo hizi kwani msimu uliopita filamu ya Kitendawili ya Richard Mtambalike ilinyakua tuzo ya filamu bora ya lugha ya Kiswahili wakati Elizabeth Michael ‘Lulu’ alivuma katika tuzo hizo katika filamu yake ya Mapenzi iliyoteuliwa kuwa filamu bora kabisa Afrika Mashariki. 

 Africa Magic Viewers' Choice Awards (AMVCA) inafanyika kila mwaka na inaandaliwa na Multichoice Africa ikiwa na lengo la kutambua na kuthamini mafanikia makubwa katika sekta ya filamu na televisheni kulingana na uchaguzi wa watazamaji.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget