HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 1 February 2017

PSPTB YATOA MAFUNZO KWA WATUMISHI WA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi ameshauri juu ya kuwepo kwa sheria ya manunuzi kwa njia ya mtandao ili kuokoa muda unaotokana na kuzunguka kwa makaratasi katika ofisi.

Profesa Janabi ameyasema hayo leo wakati akifungua mafunzo ya watumishi wa taasisi hiyo wanaohusika na manunuzi ambayo yameratibiwa na Bodi ya Manunuzi na Ugavi (PSPTB), amesema uwepo wa mafunzo hayo, utasaidia kutatua changamoto hizo.

"kuendesha manunuzi katika mtandao kutapunguza gharama ambazo zinaweza kuokoa fedha nyingi zitakazotumika katika masuala mengine" alisema Profesa Janabi.

Nae Mratibu Mkuu wa utafiti na ushauri wa PSPTB bwana Amos Kazinza, amesama kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 budget ya serikali imetenga asilimia 76 kwa ajiliya Ununuzi. Hivyo manunuzi huchukua kiasi kikubwa cha fedha. Amesema mabadiliko ya sheria yamelenga kuongeza ufanisi na kuhakikisha kwamba thamani ya fedha inapatikana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi akizungumza na wataalamu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya manunuzi ya Umma kwa watumishi wa tasisi hiyo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza na kufatilia hotuba ya ufunguzi .
Wataalamu kutoka bodi ya manunuzi na ugavi (PSPTB) wakiongozwa na afisa habari, Shamim Mdee katika mkutano huo .
Mratibu Mkuu wa Utafiti na ushauri wa PSPTB, Amos Kazinza akitoa elimu juu ya masuala ya manunuzi kwa watumishi wa tasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad