HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 20, 2017

EQUITY BANK TAWI LA MBEYA WATOA ELIMU KWA WANACHAMA WA NAMAINGO MBEYA...

Equity Bank tawi la Mbeya wakishirikiana na Kampuni ya Namaingo Business Agency wametoa mafunzo kwa wanachama wa Namaingo katika mtaa wa Block-T kata ya Iyela Jijini Mbeya kuhusiana na Elimu ya Fedha.
Akifungua Mafunzo hayo Bw.Jotham Wilson aliwaomba wanachama kuwa watulivu mafunzoni na kuuliza maswali pale watakapokuwa hawajaelewa.
Naye, Afisa Elimu ya Fedha kutoka Equity Bank Bi.Suzane David alianza kwa kuwafafanulia wanachama kwa kina huduma zitolewazo na Benki hiyo.
Aidha,Afisa huyo akitumia mfumo shirikishi katika mafunzo alifundisha njia tofauti za uhifadhi wa fedha akisema zipo zilizo rasmi kama kuweka Benki yaani kwenye taasisi za kifedha na njia zisizo rasmi za uhifadhi kama kuweka kwenye kibubu, kuchimbia chini, kuhifadhi ndani, kukopesha na VICOBA.
Bi.Suzane David alienda mbali zaidi  wakati akijibu maswali yaliyoulizwa na Bw.James Mwampagatwa,Mzee Kajigili na Bi.Felister Mlozi kuhusiana na Mikopo ya Kilimo itolewayo na Benki hiyo kwa kuwajuza kuwa Benki haitoi mkopo kwa mtu anayeanza kulima ila kwa yule ambaye amelima angalau msimu mmoja au miwili na hata hivyo wao hutoa pembejeo na sio fedha kwa ajili ya kumsaidia mkulima kufikia malengo yake.
Wanachama wa Namaingo walijifunza kuhusu Elimu ya bajeti, Jinsi ya Uwekaji Akiba na Udhibiti wa madeni ambapo Afisa Elimu ya Fedha Bi.Suzane alifafanua zaidi juu ya Mikopo mizuri na mikopo mibaya kwa kutolea mfano Mtu akopae fedha kwa ajili ya harusi kuwa huo ni mkopo mbaya kwani hauendi kuzalisha ila kwa mtu akopae kwa ajili ya kuongeza Kibanda chake cha chipsi au chochote huo ni mkopo mzuri kwani unaenda kuzalisha.
Wanachama walionekana wenye furaha muda wote wa mafunzo na wengi wao kuridhishwa na mafunzo hayo na wengine kuamua kufungua Akaunti ndani ya Benki iyo ambayo Akaunti zake zote hazina makato.
Equity Bank wana Akaunti zifuatazo:- 
1.Akaunti ya kawaida (Ordinary Account) 2. Akaunti ya malengo (Jijenge Account) 3. Akaunti ya watoto (Super Junior Account) 4. Akaunti ya Biashara 5. Akaunti ya Vikundi na Akaunti ya watu waishio nje ya nchi (Diaspora Account)


 Afisa Elimu ya Fedha kutoka Equity Bank Bi.Suzane David akitoa elimu kwa wanachama wa namaingo ukanda wa Mbeya.
Utulivu ukitawala masaa yote ya mafunzo



Mwana Namaingo akiandika mambo muhimu wakati wa Mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Elimu ya Fedha Bi.Suzane David
Wanachama wa Namaingo wakifuatilia mafunzo nje ya Ofisi ya Namaingo Business Agency iliyipo mtaa wa Block-T Jijini Mbeya
Afisa Elimu ya Fedha Bi.Suzane David akisisitiza jambo wakati akifundisha juu ya Udhibiti wa madeni
 Afisa Elimu ya Fedha kutoka Equity Bank akiongea na wanachama wa Namaingo huku mwanaHabari Yona Mgaya wa Adonai Fm Radio akichukua habari

PICHA ZOTE NA: MR PENGO MMG...

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad