HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 18, 2017

Watanzania wahamasishwa kuwekeza Falme ya kiarabu (UAE)


Mkurugenzi wa mipango na maendeleo ya baishara wa RAK International corporate centre, Bw.Shankar Bharathan akizungumza jambo na Mkurugenzi wa karimjee consultants Bi.Farzana Kajimjee. Mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichotazamia fursa za uwekezaji baina ya Tanzania na Nchi ya Falme za Kiarabu katika kituo cha RAK International corporate. Katikati ni Mshauri na Mratibu wa kituo hicho,Bw.Gaudence Kayombo.
Mkurugenzi wa mipango na maendeleo ya baishara wa RAK International corporate centre, Bw.Shankar Bharathan akitoa mada juu ya fursa za uwekezeji na biashara zilizopo katika mji wa Ras Al Khaimah katika kituo cha Rak international corporate kwa wafanyabishara na wadau wa maendeleo toka Tanzania. Mazingira ya biashara hasa katika kodi ni mazuri kwa watanzania kwenda kuweka katika nchi za falme za kiarabu.

NA MWANDISHI WETU, Dar
KINYUME na ilivyozoeleka kwa mataifa yaliyoendelea kuja kuwekeza nchini, hali imekua tofauti baada ya Serikali ya Falme za Kiarabu (UAE) kupitia mji wa Ras Al Khaimah kuwaomba Watanzania kwenda kuwekeza katika mji huo wa kitalii.

Akizungumza katika hafla ya utambulisho wa fursa za kibiashara kwenye mji huo jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Mkurugenzi wa mipango uhusiano na ushirikiano wa maendeleo ya kibiashara katika kituo cha RAK International Corporate Centre, Shankar Bharathan alisema wafanyabishara kutoka ukandahuu waende wakanufaike na uwekezaji usio na mipaka.

Alisema, kinyume na taratibu zilizowekwa na serikali ya UAE ambapo inamtaka mwekezaji kubaki na asilimia 49 huku asilimia 51 ikichukuliwa na serikali, kwa RAS Al Khaimah utaratibu huu haufuatwi, na hata mfanyabishara anapata nafasi ya kuondoka na faida yake bila kubughudhiwa.

“Mazingira ya kibishara ni mazuri, unaweza kufungua akaunti ya benki na kuhifadhi fedha zako bila bughudha pia ukitaka kurudi nazo nyumbani unaruhusiwa, tunachotaka ni kupata wawekezaji wengi katika Nyanja mbalimbali kadiri iwezekanavyo.

“UAE ni muunganiko wa miji mingi lakini mji huu upo Abu Dhabi, tunapenda kufanya kazi na Watanzania kwa sababu ni watu wakarimu pia wafanyabiashara wengi wanakuja UAE kununua vitu na kuondoka sasa tunataka wakawekeze ili na sisi tununue kutoka kwao,” alisisitiza.

Kwa upande wake mmoja wa wahudhuriaji wa hafla hiyo ya utambulisho Elinisaidie Msuri kutoka kampuni ya MEKONSULT, alisema huu ndio wakati wa Watanzania kutumia fursa ya kuwekeza katika eneo la ghuba.

“Tumekuwa tukilalamika kuhusu wawekezaji kuja nchini kuchukua maeneo na kazi zetu, fursa imejitokeza tusiiache. Masuala ya kodi hakuna kama alivyozungumza Bharathan, hata ule ubia wa asilimia 51 kuchukuliwa na serikali pia haupo.

“Hii ni biashara iliyo na faida kubwa, kwa sababu ikiwa unaruhusiwa kusafirti na pesa ulizofanyia biashara unataka nini tena, kwa sababu hiyo ndiyo changamoto kubwa kwa wafanyabishara wa kimataifa. Tutafute namna ya kutembelea mji huu ili tujionee na kujifunza namna biashara hii inavyofanyika, huenda watu wasiamini au wasielewe kilichozungumzwa lakini kuona ni kuamini. Watanzania tuamke fursa imejitokeza,” alisema Msuri.

Akizungumzia masuala ya usajili na malipo ya tozo, Bharathan alisema hakuna urasimu katika masuala kama hayo na hata ikiwa mmiliki atataka kampuni yake iwe na ushirika kutoka mataifa mengine inakubalika.

RAK International Corporate Centre ni mamlaka iliyo katika mji wa Ras Al Khaimah iliyoanzishwa kutokana na muunganiko wa kampuni mbili za RAK International Companies ambayo awali iliitwa RAK Free Trade Zone na RAK Offshore ambayo awali ilikuwa sehemu ya RAK Investment Authority.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad