Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kulia), akitoa maelekezo kwa Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Bw. Godfrey Simbeye, wakati alipokagua shughuli zinazofanywa na mfuko huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa(Kulia), akipata taarifa ya utendaji kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF Eng. Peter Ulanga, alipokagua shughuli zinazofanywa na mfuko huo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akikagua kumbukumbu za wateja wanaohudumiwa na kampuni ya simu TTCL kanda ya Kaskazini eneo la Kijitonyama jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akisisitiza jambo kwa maofisa wa kampuni ya Simu TTCL kanda ya Kaskazini alipokagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa ofisa wa kampuni ya Simu TTCL namna ya kufanya kazi kwa ubunifu ili kuongeza wateja katika kampuni hiyo. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Menejimenti ya Mfuko wa
Mawasiliano kwa wote (UCSAF), kuhakikisha vijiji vyote nchini ambavyo havijaunganishwa
na huduma ya mawasiliano vinaunganishwa
kabla ya mwisho wa mwaka huu.
Aidha, Profesa Mbarawa
amesisitiza mfuko huo kutoa kipaumbele kwa vijiji vyote vilivyomo sehemu za
mipakani ili kuimarisha ulinzi na uharaka wa mawasiliano katika maeneo hayo.
Amewaagiza UCSAF
kukutana na mitandao ya simu ili kukamilisha kazi kwa mujibu wa mkataba kwa kata 121 ambazo hazijapata huduma ya mawasiliano hapa
nchini.
“Nia ya Serikali ni kuhakikisha vijiji vyote
nchini vinapata huduma ya mawasiliano ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba ili
kuwezesha mikakati mingine ya kuboresha Mifumo ya Tehama katika shule na
Hospitali kuendelea na hivyo kuhuisha huduma za Tehama katika Sekta za afya na
elimu”, amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa
ameonya kampuni za simu zitakazoshindwa kupeleka mawasiliano katika maeneo
waliyopangiwa kwa wakati zitapokonywa masafa katika maeneo husika ili kuzipa
kampuni zilizo tayari.
Naye Mjumbe wa Bodi ya
UCSAF Bw. Godfrey Simbeye, amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa Bodi yake
imejipanga kuhakikisha inaratibu huduma zote za Tehama zinazotolewa na taasisi
mbalimbali nchini ili kuweka uwiano wa huduma hizo nchini kote.
Kwa upande wake, Mtendaji
Mkuu wa UCSAF Eng Peter Ulanga, amesema kuwa mfuko huo umejipanga kupeleka
mawasiliano katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara ili kutoa haki kwa wakazi
wa maeneo hayo kunufaika na fursa za mawasiliano na kuchochea maendeleo.
Takribani asilimia 94
ya Wakazi wa Tanzania wanapata huduma ya mawasiliano lengo likiwa ni kufikia
asilimia 100 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment