HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 30, 2016

USHINDI WAMPA JEURI ALIYECHUKUA MIKOBA YA HERNANDEZ AZAM FC.

Kiungo wa Azam Fc Joseph Mahundi akijaribu kumtoka beki wa Prison katika mchezo uliofanyika jana usiku kwenye  Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Baada ya ushindi wa jana wa goli 1-0 dhidi ya  Tanzania Prisons, kikosi cha Azam kwa sasa kinaondoka kwenda visiwani Zanzibar kujiandaa na mivhuano ya Mapinnduzi inayotarajiwa Desemba 31 huku benchi jipya la ufundi likijizatiti kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Katika mchezo huo wa ligi kuu ulikuwa ni wa mwisho kwa Azam  kabla ya kuukaribisha mwaka mpya ‘2017’,  na bao pekee la ushindi likiwekwa kimiani na nahodha John Bocco ‘Adebayor’, katika dakika ya 40 baada ya kupokea pasi safi ya Joseph Mahundi na kuwahadaa mabeki wa Prisons kisha kupiga shuti la kiufundi lililojaa kimiani.

Azam FC iliingia kwenye mchezo huo ikiwa na sura mpya kwenye benchi la ufundi lililosimamiwa na makocha wa timu yake ya vijana, Idd Nassor Cheche na Idd Abubakar na hii ni kufuatia kuwasitishia mikabata wakufunzi kutoka Hispania wakiongozwa na Kocha Mkuu, Zeben Hernandez na h

uo ni ushindi wa kwanza wa Azam FC kwenye mechi za mzunguko wa pili wa ligi baada ya kuanza vibaya kwa kutoka sare mechi mbili mfululizo dhidi ya African Lyon (0-0) na Majimaji (1-1).


Kocha Iddy Nassor Cheche amesema kuwa, kwa sasa anachokiangalia ni kuweza kuisaidia timu yake kuweza kufanya vizuri kwenye kombe la Mapinduzi na si vinginevyo na zaidi ana imani na kikosi che kwani kinaweza kufanya vizuri ya mchezo wao dhidi ya Prison.

Azam FC kwa sasa inaelekea kwenye changamoto nyingine ya kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo itaanza kufungua dimba Jumatatu ijayo kwa kucheza na Zimamoto saa 10.15 jioni ndani ya Uwanja wa Amaan, visiwani Zanzibar wakipangwa katika kundi moja na mabingwa watetezi wa ligi kuu Yanga huku mechi yao ikitarajiwa kuwa Januari 06.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad