HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 2, 2016

REDIO DREAM FM 91.3 MBEYA KUHITIMISHA MASHINDANO YA GREEN CITY ENTER-COLLEGE HII LEO UWANJA WA TIA JIJINI MBEYA..

Mashindano ya Green city Enter-College yanayoshilikisha Vyuo vikuu vya kati vilivyopo jijini mbeya yanatarajiwa kumalizika Ijumaa ya leo jijini mbeya tangu kuanza kwake siku ya Jumamosi ya  tarehe 26 novemba mwaka huu, Mashindano hayo ya Enter-College yaliyo andaliwa na kituo cha Redio Dream Fm 91.3 Mbeya pia kupewa nguvu na Mamlaka ya usimamizi wa Hifadhi ya sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA), Kilimanjaro Premiam Lager,  Ally Rich sanaa (ARTS) na Michuzi Media, Yamelenga zaidi katika kuwapatia fursa wanafunzi wa vyuo vikuu na kati kukutana kwa pamoja na kuendeleza vipaji vyao, kuwajenga wanafunzi kupenda michezo na kufanya mazoezi, Kuepukana na mambo yasiyo faa katika jamii na kukemea vitendo visivyo rafiki na jamii yetu, Vyuo vilivyo shiriki katika bonanza hilo la mashindano ya mpira wa miguu na mpira wa pete kwa vyuo vikuu na kati jijini mbeya ni Chuo cha uwasibu mbeya (TIA), Theofilo kisanji (TEKU), St.Agustene (SAUTI), Chuo cha elimu ya biashara (CBE), Chuo cha sayansi na teknolojia (MUST), Tumaini Makumira, Chuo cha Kilimo Uyole na Veta, Ambapo kila chuo Kimeshiriki na kupewa jezi na mipira kwa wavulana na wasichana.
Mashindano hayo ya Enter-College yatamalizika leo katika Uwanja wa chuo cha Uwasibu (TIA) jijini mbeya ambapo Zawadi za washindi zitatolewa na baada ya hapo sherehe ya kufunga mashindano hayo iliyopewa jina la (Green City Inter-College Back to Campus Bush) itafanyika katika Ukumbi wa Club K moo zamani kiwila motel, shafra Iliyo ambatanma na Burudani mbalimbali ikiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wanavyuo wenye vipaji,
 Kutoka kushoto ni meneja mkuu wa Redio Dream fm 91.3 iliyopo mkoani mbeya ndugu, Grayson Kayombo akikabithi uzi kwa Kiongozi wa michezo chuo cha St.Augustine (SAUTI) bwana Katuli Francis Kabla ya mashindano kuanza.


 meneja mkuu wa Redio Dream fm 91.3 iliyopo mkoani mbeya ndugu, Grayson Kayombo akizungumza na baadhi ya timu zilizoshiliki mashindano hayo.
 meneja mkuu wa Redio Dream fm 91.3 iliyopo mkoani mbeya ndugu, Grayson Kayombo Akisalimiana na baadhi ya wachezaji walio shiriki Mashindano hayo yaliyoandaliwa na kituo cha Redio Dream Fm 91.3 Mbeya pia kupewa nguvu na Mamlaka ya usimamizi wa Hifadhi ya sekta ya hifadhi ya jamii (SSRA), Kilimanjaro Premiam Lager, Ally Rich sanaa (ARTS) na Michuzi Media.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad