Mtaa Kwa Mtaa Blog

JAVIS WAJIZATITI KUONGEZA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA NCHINI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
JAVIS wapania kuendela kutoa fursa kwa vijana ili kuweza kujikomboa kutoka katika limbi la umasikini na vijana hao wataleta mabadiliko ya kibiashara wenye mikakati ya kuleta mapinduzi kwenye jamii, hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo Haruna Marwa Elius wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na wateja wao.

Elias amesema kuwa kwa sasa wameshasaa zaidi ya mikoa mitano nchini na wametoa elimu kwa vijana na tayari wameshapata fursa ya kazi pia nao wamepewa jukumu la kutoa elimu kwa vijana wengine.

Javis ni kampuni inayoendeshwa na vijana inajihususha na masuala ya usafirishaji mizigo kutoka nchini China na tayari imeshafungua matawi yake katika maeneo tofauti, huku lengo kubwa ikiwa ni kuwasaidia vijana kuweza kujiingiza katika kufanya biashara itakayokuwa na faida kwao.

Afisa Masoko wa Javis Steven Gerald amesema kuwa,kuna changamoto mbalimbali katika kuendesha biashara zao ikiwemo kuchelewa kwa meli, kuchelewa kutoka bandarini muda mwingine bidhaa kufika zikiwa zimeharibika. 

Gerald amesema kuwa wamejipanga kuweza kuhakikisha wanazidi kuvuka mipaka kwani mpaka sasa wana tawi lipo Guanzhu nchini China na lenyewe kule linasaida pindi wateja wanapoenda kununua bidhaa wanune kutoka viwandani au kwa mawakala wanaojulikana na sio katikamaduka ya kawaida.
 Mkurugenzi wa kampuni ya Javis Haruna Marwa Elius akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na wateja wao kutoka maeneo mbalimbali na kutokea ufafanuzi jinsi kampuni yao inavyofanya kazi.
 Afisa Masoko wa Javis Steven Gerald akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na wateja wao kutoka maeneo mbalimbali na kutokea ufafanuzi jinsi kampuni yao inavyofanya kazi..

Mwenyekiti au muandaaji wa hafla baina ya Javis na Wateja wake akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na wateja wao kutoka maeneo mbalimbali na kutokea ufafanuzi jinsi kampuni yao inavyofanya kazi
Baadhi ya wateja waliojotokeza kwenye hafla hiyo wakiwa makini kusikiliza
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget