Msajili wa Hazina, Lawlance Mafuru akizungumza na waandishi wa habari juu hali ya mzunguko wa fedha leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema mzunguko wa fedha sio mzuri kutokana na fedha nyingi kwenda katika miradi ya kuimarisha huduma kwa wananchi.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es
Salaam, Msajili wa Hazina, Lawlance Mafuru wakati akizungumza na waandishi
habari juu ya taarifa zinazosambaa zinazodai kuwa benki zimeyumba.
Amesema serikali katika kudhibiti
fedha za umma katika mashirika na taasisi ni kuwa na akaunti benki kuu ili
kuweza fedha hizo kuonekana na sio kuwa katika benki zingine.
Mafuru amesema kuyumba kwa taasisi za
fedha haitokani na kuondolewa kwa kiasi
cha sh.bilioni 515 kwa kila taasisi kuwa na akaunti benki kuu.
Amesema taasisi za fedha kwa septemba
zimekopesha sh.trioni 16 kati ya fedha hizo sh.trioni 1.4 ni mikopo mibovu
hivyo kwa benki lazima ziyumbe kwa muda kutokana na mikopo hiyo mibovu.
Mafuru amesema kupanga ni kuchagua
hivyo serikali imetaka kuimarisha huduma kwa wananchi , lazima kuwekeza kwa
kiasi kikubwa katika huduma za kijamii.
Amesema viwanda vikijengwa hapa nchini wananchi watanunua bidhaa za ndani hivyo fedha itazunguka hapa hapa kuliko
kununua bidhaa za nje ambazo fedha zinakwenda kuwapa maendeleo nchi nyingine.
Aidha amesema kuwa nia Rais Dk. John
Pombe Magufuli ni njema ya kutaka kuimarisha huduma kwa wananchi katika miradi
mbalimbali zinazokusanywa.
No comments:
Post a Comment