HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 30, 2016

BALOZI WA KUWAIT NCHINI ATEMBELEA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE


Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimkabidhi zawadi ya dawa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi ambazo zitatumika kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Prof. Ayoub Magimba na Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.
Na Anna Nkinda - JKCI

Serikali ya Kuwait imeahidi kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu , mashine  na vifaa vya upasuaji ambavyo vitatumika katika chumba cha upasuaji.

Ahadi hiyo imetolewa leo na  Balozi wa nchi hiyo Mhe. Jasem Al Najem alipotembelea  Taasisi hiyo kwa ajili ya kuangalia ni  jinsi gani nchi yake inaweza kuisaidia katika upatikanaji wa vifaa  tiba.

Mhe. Balozi Al Najem alisema vifaa vitakavyotumika katika utunzaji na utoaji wa damu vitapatikana kabla ya kumalizika  kwa mwaka huu ambapo vifaa  pamoja na mashine za upasuaji vitapatikana mwanzoni mwa mwaka ujao wa 2017.

“Serikali ya nchi yangu inaangalia namna ya kushirikiana zaidi na Taasisi hii pamoja na Taasisi zingine zilizopo Dar es Salaam, Zanzibar na maeneo mengine hapa nchini ili watanzania waweze kupata huduma bora”, alisema Mhe. Balozi Al Najem.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi  alishukuru Serikali ya Kuwait kwa kuahidi kuwapatia vifaa pamoja na mashine  zitakazotumika katika matibabu ya wagonjwa wa moyo.

“Tuna vyumba vitatu vya upasuaji, vinavyotumika ni viwili kwani kimoja hakina vifaa, kupatikana kwa vifaa pamoja na mashine kutoka nchini Kuwait kutatufanya tuwe na vyumba vya upasuaji vitatu ambavyo vitasaidia  kutoa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa .

Akiwa katika Taasisi hiyo Mhe. Balozi Al Najem alitembelea vyumba vya upasuaji wa moyo, chumba cha wagonjwa walioko katika uangalizi maalum (ICU) na kutoa  zawadi kwa watoto waliolazwa.
Daktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuelezea takwimu za upasuaji wa wagonjwa wa Moyo zinazofanywa na Taasisi hiyo Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem (kushoto). Wapili kulia ni Dkt. Barjces Almutairi kutoka Mfuko wa Kusaidia wagonjwa wa nchini Kuwait akifuatiwa na Daktari Bingwa wa Moyo Tulizo Shemu Sanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam ili kuona namna gani nchi yake inaweza kusaidia vifaa tiba.

Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya gari na ndege ya kuchezea Mtoto Jumanne Mndeme ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya matibabu ya moyo huku Mama yake Jumanne akishuhudia.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiongea jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati balozi huyo alipotembelea Taasisi hiyo na kuahidi kuisaidia vifaa vya kutunzia damu na kununua vifaa kwa ajili ya upasuaji wa moyo katika chumba cha upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Moyo Peter Kisenge.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akimpa zawadi ya mdoli Mtoto Furaha Mwechi ambaye amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa ajili ya kuziba tundu la moyo na kufungua mshipa wa damu kutoka kwenye moyo kwenda kwenye mapafu. Mhe. Balozi Najem alitembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam ili kuona ni jinsi gani nchi yake inaweza kuisaidia vifaa tiba.

Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Ubalozi wa Kuwait mara baada ya kumalizika kwa ziara yake aliyoifanya katika Taasisi hiyo. Kulia kwa Mhe. Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji JKCI Prof. Mohamed Janabi.
Balozi wa Kuwait Nchini Mhe. Jasem Al Najem akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam ili kuona ni jinsi gani nchi yake itakavyoisaidia Taasisi hiyo. Kulia kwa Balozi ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi. Picha na Anna Nkinda – JKCI.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad