
Bidani mwenye urefu wa futi saba akiwa na rafiki zake katika eneo la Kayaking walifika karibu na eneo la uvunjwaji wa shimo hilo la mchanga ikiwa inakadiriwa kuwa na urefu wa mita 50 hadi 80 kwenda chini na kufukiwa huku wenzie wakiokolewa na yeye mwili wake ukiwa haujapatikana mpaka muda huu.
Ajali hiyo imetokea Jumatatu usiku, Sheriff Jerome Kramer amesema mwili wa Bidan bado haujapatikana kwani kuna kiasi kikubwa cha mchanga katika eneo hilo na wanahisi kuwa kwamba uwezekano mkubwa wa kuwa kafunikwa na mchanga.
Wafanyakazi wa eneo hilo wametumia muda mwingi kuzuia uvunjaji wakiwa na matumaini ya kuacha mtiririko ili kupunguza kiasi cha uchafu katika maji. Wakati huo huo, boti mbalimbali zinaendelea kutafuta mwili wa Bidan. Kramer anasema wao wanatambua eneo ambako alikwenda ndani ya maji, hivyo wanaendelea kutafuta eneo hilo sana.

Bidan, ni moja ya wacheza mpira wa kikapu nchini humo na tayari alikuwa amepangwa na Kocha wake Kevin O'Connor katika timu ya chuo cha North Platte Community. Dk Jody Tomanek, Makamu wa Rais wa North Platte Community College, alisema, "Hii ni ya kusikitisha na kutisha sana, ni pigo kubwa tumelipata kama chuo, Katika muda mfupi Samson alikuwa pamoja na wenzake Chuoni na amekuwa kivutio kwa wanafunzi na wafanyakazi."
No comments:
Post a Comment