Katikati ni Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U-17), Serengeti boys, Bakari Shime kulia ni Mkufunzi wa soka la Vijana hapa nchini, Kim Poulsen na Kushoto ni Kiongozi wa TFF wakijadiliana jambo jana katika kiwanja cha Karume jijini Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
TIMU ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 (U-17), Serengeti boys imesema ipo fiti kuwavaa Washelisheli katika mchezo wao wa kimataifa unaotarajiwa kuchezwa Juni 26 huku waamuzi wakitokea nchini Ethiopia.
Mwamuzi wa kati katika mchezo huo ni Belay Tadesse Asserese atakayesaidiwa na Tigle Belachew, Kinfe Yilma kinfe, Lemma Nigussie atakuwa mwamuzi wa mezahi huku kamisaa wa mchezo huo Kalombo Bester akitokea nchini Malawi.
Akizungumzia maandalizi hayo kocha mkuu wa timu hiyo Bakari Shime amesema kuwa kitu kikubwa katika mchezo huo ni ushindi si vinginevyo. Toka timu yake iingie kambini Juni 14 mwaka huu wamefanya kazi kubwa ya kuwaandaa vijana kisaikolojia ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo.
"Kwa ushirikiano mkubwa wa bechi la ufundi la timu hii tumeweza tumeshirikiana vema na mwalimu Kim Polsen vijana wameonesha morali kubwa ya mchezo huo, maandalizi tuliyoyafanya toka kuingia kambini hadi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Shelisheli matumaini makubwa yapo katika ushindi kwani hatuwazi kupoteza kwa namna yoyote ile ", amesema Shime. Aidha Shime amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa hamasa vijana ya kufanya vizuri.
Serengeti ni timu pekee ya Taifa iliyobaki katika mashindano ya kimataifa baada ya timu ya wakubwa, Kilimanjaro Stars kupoteza mchezo wake dhidi ya Wamisri na Stars sasa italazimika kucheza mchezo wake wa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria ili kukwepa rungu la FIFA.
No comments:
Post a Comment