HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 21, 2016

HADHARANI WAAMUZI WA YANGA VS TP MAZEMBE.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetoa ratiba ya waamuzi watakaocheza mechi ya Yanga dhidi ya TP Mazembe, mechi itakayopigwa Juni 28 katika dimba la uwanja wa Taifa ambao utachezeshwa na mwamuzi kutoka nchini.

Zambia John Sikazwe akisaidiwa na Jersom Emiliano Dos Santos kutoka Angola pamoja na Berhe O'Michael wa Eritrea huku mwamuzi wa akiba akiwa Wellington Kaoma kutoka Zambia. Kamisaa wa mchezo huo atakuwa ni Celestine Ntagungira kutoka Rwanda.

Yanga itavaana na Mazembe huku ikiwa imetoka kupoteza mchezo wake wa awali dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria kwa kukubali kichapo cha goli 1-0.

Katika mchezo huo Yanga walitengeneza nafasi kadhaa lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo na kupelekea kupoteza mchezo huo wa awali.Ushindi huo unaifanya MO Bejaia kushika nafasi ya pili katika kundi A nyuma ya Mabingwa wa Afrika TP Mazembe huku Yanga ikishika nafasi ya tatu.

Mchezo unaoikutanisha miamba hiyo ya soka unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na Yanga kuyhitaji ushindi katika mchezo wake wa kwanza nyumbani katika mashindano hayo. Kwa sasa Yanga wamerejea kambini nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi dhidi ya mazembe huku wakitarajiwa kutua nchini siku mbili kabla ya mchezo wao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad