HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 21, 2016

TFF yawapongeza Wambura na Kambi.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
RAISI wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi (Pichani)ametuma salamu za pongezi kwa Katimu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka nchini (FAT sasa TFF), Michael Wambura kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM).

Wambura ambaye ni Kamishna wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa FAM baada ya kupata kura 26 kati ya 27 zilizopigwa. Katika uchaguzi huo Wambura hakua na mpinzani katika nafasi hiyo kwa uchaguzi uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Musoma Mjini.

Mbali na kumpongeza Wambura Malinzi pia ametusa salamu zake za pongezi mwa Mwenyekiti mypa wa Chama cha mpira wa Miguu mkoani Mtwara, Bw. Kambi

Akizungumza kwa niaba ya Malinzi, Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kuwa Malinzi ni matumaini yake kuwa viongiozi hao watazitumikia vema nafasi zao.

Alisema, kwa kipindi kirefu soka limeshindwa kuongozwa vizuri katika ngazi za mikoa hivyo kupitia wao mambo huenda yakabadilika. "Ni matumaini ya Rais kuwa viongozi hao watasimamia vema michezo na kukuza soka la sehemu walizopo ili kuhakikisha zinakuwa mfano wa kuigwa", amesema Alfred.

WAKATI HUOHUO.
Twiga Stars  kuwekwa wazi mwisho wa mwezi huu.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania (Twiga stars) kinatarajiwa kuwekwa hadharani mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya  kuingia kambini siku 10 kabla ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda huku wakipatiwa mwalimu maalumu kutoka nchini Rwanda kwa ajili ya maandalizi ya timu yake kuelekea katika mashindano ya fainali za mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake.

Rwanda ilituma mwaliko huo kutokana na kiwango kizuri walichokionesha Twiga katika michezo yake mbalimbali ya kimataifa waliyoicheza.

Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Alfredy Lucas amesema mchezo huo ni mwaliko maalumu kutoka kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa ajili ya kuwapa burudani viongozi watakaohudhuria mkutano mkuu wa nchi za Afrika AU.Mkutano huo unatarajiwa kuanzia Julai 14 mpaka 16 mwaka huu hivyo anataka kuonesha viongozi hao kuwa hata wanawake wanaweza.

Amesema, kwa kipindi kirefu wanawake wamechukuliwa kama viumbe dhaifu hivyo mchezo huo utasaidia kuondoa fikrea hizo.
"Tunatumai kuwa Twiga wataonesha kiwango kizuri katika mchezo huo na kuleta ushindani mkubwa ili kudhihirisha kuwa si wanaume tu ndio wanaoweza kusakata kabumbu bali hata wanawake wanauwezo mkubwa katika mchezo huo", amesema Alfred.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad