Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KLABU ya Yanga katika kuimarisha kikosi chake kimepania kufanya usajili wa kimataifa kwa ajili ya michuano ya kombe la Shirikisho Afrika hatua ya nakundi pamoja na ligi kuu msimu ujao kwa kusaka saini ya mshambuliaji wa kimataifa Obrey Chirwa(Wapili kutoka kulia) kutoka nchini Zambia anayekipiga kwenye kikosi cha FC Platinum. Mshambuliaji huyo muda wowote atatangazwa kukamilisha uhamisho kujiunga na Yanga.
Chirwa anatarajiwa kuwasili leo kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kujiunga huku ikisemekana Yanga wamelazimika kulipa zaidi ya Milioni 200 kupata saini yake na wana matumaini makubwa kuwa Chirwa atafanya vizuri kama walivyofanikiwa wachezaji wenzie wa zamani wa FC Platinum Donald Ngoma na Thabani Kamusoko.
Chirwa alijiunga na FC Platinum misimu miwili iliyopita lakini mwaka jana alipata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Horbo IK ya Denmark ila baada ya kutovutiwa na maslahi aliamua kuachana nayo na kisha akaamua kurudi timu yake ya awali FC Platinum. Mitandao ya nchini Zimbabwe inaandika kuwa Chirwa ameondoka jana na amekuja nchini Tanzania kumalizia makubaliano ili kuweka dole gumba kwa wanajangwani hao huku Mkuu wa Kitengo cha habari wa Yanga, Jerry Muro akiweka kuwa bado wana mikakati pia na Mshambulaji mwingine wa timu hiyo Mussona.
Yanga kwa sasa wapo nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa ufunguzi wa kombe la Shirikisho dhidi ya Mo Bejala unaotarajiwa kupigwa Juni 19 saa nne usiku na kisha kurejea tena Uturuki ambapo Chirwa ataungana nao.
No comments:
Post a Comment