HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 16, 2016

UJUMBE WA MISS TANZANIA 2016/2017 WAKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO.


Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Miss Tanzania, Lilian Kamazima  mara baada ya kumalizika kwa kikao cha baadhi ya wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa mikutano wa TBC mjini Dodoma. Kikao hicho kilijadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuiomba Serikali iwasaidie kupata wadhamini wa mashindano hayo kitaifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa kikao  baina yao kilichofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Shirika la  Utangazaji la Taifa (TBC) mjini Dodoma.
Mhe. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wajumbe wa kamati ya Miss Tanzania 2016/17 mara baada kumalizika kwa kikao  baina yao kilichofanyika   mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) mjini Dodoma. 
Picha na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad