HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 16, 2016

TIMU YA TAIFA NCHIN I TOGO YAMWITA MCHEZAJI, BOSSOU (YANGA).

Zainab Nyamka.
KOCHA mpya wa Togo Mfaransa Claude LeRoy amemuita Vicent Bossou(Pichani) katika kikosi cha timu yake ya Taifa baada ya kumuangalia katika mechi alizocheza na  klabu yake ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika na ligi kuu Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotufikia kutoka kwa Katibu mkuu wa chama chama cha Mpira wa miguu nchini Togo, Pierre Lamadokou, amesema kuwa barua ya mchezaji huyo ya kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa imeshafika  kwenye uongozi wa Yanga katika ofisi ya katibu Mkuu, Baraka Deusdedit kuwa beki huyo anatakiwa kujiunga na timu yake pindi itakapoingia kambini wiki chache zijazo kuumana na Liberia.
  
“Kweli nimeitwa kujiunga na timu ya taifa, Yanga wameshapokea barua hiyo ya mualiko na kunijulisha, kwangu ni taarifa nzuri kwa kuwa nakwenda kulisaidia taifa langu baada ya kuisaidia klabu yangu kutwaa ubingwa sasa najiunga na taifa langu,” amesema Bossou.

Mwenyewe ameonesha furaha kubwa sana kuungana na wenzake kuisaidia timu yake ya Taifa hasa baada ya kocha wa awali kutokumpa nafasi  na kuishia kusugua benchi.

Mara ya mwisho kwa Bossou kuitwa Togo ni wakati kikosi hicho kilivyokuwa kikicheza na Uganda wakati huo ikifundishwa na kocha Mbelgiji Torm Saintfiet ambaye hata hivyo hakumchezesha hata mara moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad