Uzinduzi
wa Dar Kavasha Club pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kujifunza
Kilingala utafanyika leo tarehe 05-Sep-2015 kuanzia saa 12
jioni katika ukumbi wa MRC Mikocheni, ukumbi ulio nyuma ya Shopperz
Plaza. Uzinduzi huo utasindikizwa na burudani kutoka kwa wana
Bana Marquis bendi inayoongozwa na mwanamuziki Tshimanga Kalala Assosa,
ambaye pamoja na kuwa ni kati ya wanamuziki waliokuweko katika enzi ya
uanzishwaji na ukuaji wa mtindo wa Kavasha, akiwa mwanamuziki wa bendi
kama Negro Success, Lipualipua, Orchestra kamale, na Orchestra Fuka
fuka.
Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.
Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.
Kiingilio cha onyesho hili ni BURE. Na hakika tukio hili ni la aina yake katika tasnia ya muziki wa dansi
No comments:
Post a Comment