Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusina na Msanii wa Afrika Kusini,Sipho Mwakabane ambaye atatumbuiza katika tamasha Oktoba 4 mwaka huu. Pia amesema kuwa msanii huyo wa nyimbo za Injili wa kimataifa. Na kulia ni Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga.
Mratibu wa Tamasha la kuombea Amani, Hudson Kamoga akizungumza na waandishi wa habari leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salam amesema kuwa watanzania wote bila kujali kabila, rangi na dini zote wajitokeze katika tamasha hilo la kuombea amani ambapo viingilio ni sawa na bure kabisa watu wazima kwa nafasi ya VIP wataingia kwa shilingi elfu tano (5000), kawaida elfu tatu (3000) na watoto ni shilingi elfu moja(1000)
Baadhi ya waandishi wa habari wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama leo jijini Dar es Salaam.
KAMATI
ya maandalizi ya Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imesema kuwa Mwimbaji wa nyimbo za Injili wa Afrika kusini, Sipho Mwakabane kuwa atashiriki tamasha la kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu ili uwe wa amani na utulivu.
Ameyasema hayo wakati akizungumza
na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha
hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama.
"Watanzania
tunatakiwa tujitokeze kwa wingi katika ufanikishaji wa tamasha hilo
ambalo linatakiwa kuwa na tamko moa la amani kuelekea uchaguzi mkuu
ambao utahusisha nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais," alisema Msama.
Alisema
baada ya kumalizika jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo
litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba
11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora),
Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).
No comments:
Post a Comment