HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 19, 2015

BENKI YA DCB YAKUTANISHA VIONGOZI WA SACCOS JIJINI DAR ES SALAAM

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BENKI ya DCB imekutanisha viongozi wa  mifuko ya kuweka na Kukopa (SACCOS) kuweza kuwapa fursa mbalimbali zilizopo katika benki hiyo.
Akizungumza na viongozi wa SACCOS, Meneja Mwandamizi wa Biashara Ndogo na Kubwa, Haika Machaku, amesema benki ya DCB iko karibu na SACCOS katika kupata fursa za utuzaji wa Amaana na huduma mbalimbali kwa gharama  nafuu.

Amesema wataendelea kushirikiana  na SACCOs kuangalia watavyoweza kusaidiana katika kuimarisha saccos pamoja na wanachama kunufaika na mikopo katika benki hiyo.

Aidha amesema kuwa  nia ya benki kuahakikisha wanachama wananufaika na benki  katika kuendeleza maisha kupitia fursa ambazo benki imeanisha kuinua wajasiriamali  pamoja na ushirika ikiwemo SACCOS.

Benki imewataka viongozi wa SACCOs  kufungua akaunti katika benki hiyo katika kuweza kuanza kufanya kazi  kwa ushirikiano na fursa zao ziweze kuwafikia wanachama.
 Meneja wa Mwandamizi wa Biashara Ndogo na Kubwa wa Benki ya DCB,Machaku,akizungumza na viongozi mbalimbali wa Saccos juu  ya fursa zinazopatikana katika benki ya DCB leo Makao Makuu ya DCB jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko wa Benki ya DCB, Boyd Mwaisame akizungumza na viongozi wa SACCCOs  jinsi watavyoshirikiana katika kuinua SACCOs,leo Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa SACCOS ya Wafanyakazi wa TRL,Gwammy Mwakangale Akichangia maada katika mkutano wa DCB  juu ya faida zinaziopatikana katika benki hususani mikopo ya nyumba leo Makao Makuu ya DCB,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki  ya viongozi wa SACCOs wakiwa katika mkutano ulioitishwa na benki ya DCB kuwapa fursa zinazopatikana katika benki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad