HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 14, 2015

WALIOFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MAFURIKO JIJINI DAR SASA WAFIKIA KUMI NA TATU

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kuwepo kwa mtu mmoja mwanaume aliyetambulika kwa jina la EXAVERY S/O MICHAEL, Miaka 19, Mkazi wa Kingugi Mbagala, aliefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akiwa katika harakati za kuvuka mto Kizinga, na kufikia idadi ya Watu 13 waliopoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na athari ya mafuriko kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha. 

Tukio hili lilitokea tarehe 13/05/2015 majira ya saa nane kamili mchana huko maeneo bonde la Mto Kizinga Kata ya Kiburugwa Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam. Maiti yake iliopolewa na wasamaria wema na imehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uchunguzi na utambuzi.

Nawashukuru wananchi kwa namna wanavyojitolea na kushiriki kushughulikia maafa yanayoendelea kutokea ikiwa ni matokeo ya mafuriko yaliyosababisha na mvua zinazonyesha mfululizo katika jiji la Dar es Salaam.

Nawaomba wakazi wa maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam waendelee kuchukua tahadhali kwa kuwa madhara zaidi yanaweza kutokea kutokana na kwamba mvua bado zinaendelea kunyesha. Aidha, waendelee kutoa taarifa pindi wanapoona hali yoyote isiyo ya kawaida ili hatua za haraka ziweke kuchukuliwa.

KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
S. H. KOVA
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad