Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa wapili kutoka kushoto akiwa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wa kwanza kushoto, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph Nyamhanga wakiwa wanakagua mabanda ya maonesho ya sekta ya ujenzi katika viwanja vya mlimani city jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa kulia akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kufungua mkutano mkuu wa Bodi ya Wakandarasi nchini CRB uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi nchini.
Msajili wa Bodi ya Wakandarasi nchini Eng.J. Malongo akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.
Baadhi ya wahandisi wakila kiapo katika taaluma yao ya Uhandisi kabla ya kufunguliwa kwa Mkutano huo.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa akimkabidhi zawadi Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara TANROADS Eng. Patrick Mfugale mara baada ya Taasisi hiyo kuchaguliwa kuwa mwajiri bora katika Sekta ya Ujenzi iliyotolewa na CRB.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa akisoma hotuba na kufungua rasmi mkutano wa mwaka wa Bodi ya Wakandarasi nchini CRB.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akizungummza katika mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi nchini Consolatha Ngimbwa akimkabidhi tuzo Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa kwa kuonesha kuthamini kwake katika sekta ya Ujenzi nchini.
Wajumbe wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji majenzi wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa.Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.
No comments:
Post a Comment