Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akimkabidhi mkuu wa wilaya Nyamagana Baraka Konisaga, moja ya kompyuta 25 zilizotolewa msaada kwa hospitali ya Sekou Toure leo asubuhi.
Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza jambo na Meneja Mkuu
wa Tigo Diego Gutierrez, katikati ni Mwenyekeiti wa bodi ya hospitali
ya Sekou Toure Christopher Mwita Gachuma.
Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini Mwanza mara baada ya kuto msaada wa kmpyuta kwa hospitali ya Sekou Toure leo asubuhi.
Meneja mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akibadilishana mawazo na mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bw Baraka Konisaga.
Meneja mkuu wa Tigo Diego Gutierrez akijadiliana jambo na mwenyekiti wa
bodi ya Hospitali ya Sekou Toure Christopher Mwita Gachuma, kati kati ni
meneja wa kanda ya ziwa Ally Maswanya.
Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo kwa kushirikiana na kampuni ya Huawei leo wameipatia msaada wa Kompyuta 25 zilizounganishwa na intaneti hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure.
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kwamba msaada uliotolewa kwa hospitali hiyo ya rufaa ni katika kutekeleza mkakati wa kampuni ya Tigo wa kuyabadilisha maisha ya Watanzania ili kuwa ya kidijitali katika maeneo yote, sekta ya afya ikiwa ni mojawapo.
Akiongea wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez amesema kwamba msaada uliotolewa kwa hospitali hiyo ya rufaa ni katika kutekeleza mkakati wa kampuni ya Tigo wa kuyabadilisha maisha ya Watanzania ili kuwa ya kidijitali katika maeneo yote, sekta ya afya ikiwa ni mojawapo.
“Kampuni ya Tigo inajulikana kwa kuwekeza katika miradi tofauti ya kijamii kupitia katika kitengo cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambapo tunaiwezesha jamii kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika Nyanja zote,” alisema Diego.
Aliongeza kwamba ni kwa sababu hii walilichukulia kwa uzito unaostahili ombi la hospitali ya Sekou Toure, “hatukusita kutoa msaada huu, maana tunafahamu kwamba tulichotoa kitasaidia sio tu kuboresha makusanyo ya pesa, bali pia italeta ufanisi katika usimamizi wa hospitali kwa ujumla,” aliongeza Diego.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Huawei Zhang Yongquan alisema kwamba msaada huu unaonyesha jinsi ambavyo kampuni yake imejitolea kusaidia sekta ya afya ili iendane na mabadiliko ya kiteknolojia.
“Kupitia mradi wetu wa kuweka daraja linalounganisha maendeleo ya kidijitali, Huawei tunaamini kwamba upatikanaji wa huduma za afya ni kitu muhimu kwa maendeleo ya nchi ambazo tumekuwa tukitoa huduma zetu, Huawei tuko imara katika kujenga daraja la teknolojia ambalo linaongeza ufanisi wa hospitali kupitia maboresho ya teknolojia,” alisema Zhang.
Aliongeza kwamba Huawei imekuwapo Africa kwa zaidi ya miaka 17, ikishirikiana na makampuni mbalimbali ya kizalendo ikiwamo Tigo, ambapo wamefanikiwa kuunganisha maeneo mbalimbali ya Tanzania kupitia tenolojia ya habari na mawasilaino (ICT) na wakati huo huo wakiwasaidia wananchi katika maeneno ambayo Huawei inastoa huduma zake.
Hafla hiyo ya makabidhiano ilihudhuriwa pia na mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo, ambapo alitoa wito kwa sekta binafsi kusaidia serikali katika miradi mablimbali ya afya nchini.
“Ninawashukuru sana Tigo na Huawei kwa msaada huu mkubwa kwa hospitali ya Sekou Toure, na ninawaomba wafanyabiashara wengine waunge mkono jitihada hizi kwa kujitokeza na kusaidia jitihada mbalimbali za serikali katika kuboresha huduma ya afya nchini,” alisema Muhongo.
Akipokea msaada huo, Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dr Onesmo Rwakyendera alisema kwamba kompyuta hizo zitaisaidia hospitali katika kufuatilia matokeo ya uchunguzui wa magonjwa mbalimbali, matumizi ya madawa na vifaa tiba vinavyoletwa hospitalini hapo pamoja na mambo mbalimbali ya kiutawala katika hospitali hiyo.
“Tuna imani kwamba vifaa hivi vitatupatia taarifa kamili za mapato na matumizi yetu ya kila siku, vifaa hivi pia vitatupatia taarifa ya yale yanayoendelea katika ulimwengu wa matibabu ikiwamo utafiti na pia masomo kutoka mbali,” aliongeza Dr Rwakyendera.
No comments:
Post a Comment